Habari za Punde

LEYLA RASHID KUCHUANA NA ISHA MASHAUZI JUMAMOSI HII

Kuelekea mpambano wa waimbaji nyota wa taarab malkia Leyla Rashid na Isha Mashauzi wanaotamba na vibao vyao vya “Sura Surambi” na “Nina Moyo Sio Jiwe”
Onyesho hilo linalosubiriwa kwa hamu kubwa linatarajia kutafanyika Jumamosi ya tarehe 22 mwezi huu ndani ya ukumbi wa Dar Live Mbagala jijini Dar es Saalam.
Katika pambano hilo bendi mbili kubwa za taarab, Jahazi Modern Taarab na Mashauzi Classic ndiyo zitakazosindikiza mpambano wa mahasimu hao wawili.

“Sura Surambi” ni moja ya nyimbo ambazo piga ua lazima iwe kweye ratiba ya Isha Mashauzi wakati iwe isiwe Leyla naye lazima awapagawishe mashabiki wake kwa kibao cha “Nina Moyo Sio Jiwe”.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.