Habari za Punde

MAKAMBA AZIPONGEZA KAMATI ZA VIJIJI ZA MAZINGIRA WILAYANI KILOLO

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akipata maelezo kutoka kwa Bw. Mutagabaya Mtaalamu  kutoka maabara maalumu ya kutunza Vyura ya Kihansi. 
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akihutubia wananchi wa Kijiji cha Mwantasi Wilaya ya Kilolo Mkoani Iringa, aliposimama akiwa katika ziara ya kikazi ya kukagua masuala ya mazingira.
Mjumbe wa Kamati ya Mazingira ya Kijiji cha Mwantasi Wilaya ya Kilolo Mkoani Iringa akipokea kiasi cha Shilingi laki moja zilizotolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba kuchangia Mfuko wa Mazingira wa Kijiji.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba na ujumbe wake wakikagua mitambo ya kusukuma maji katika Mkoa wa Iringa, wa kwanza kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bi. Amina Masenza.
*************************************************
Na Lulu Mussa, Kilolo - Iringa 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba amesisitiza umuhimu wa kutunza Vyanzo vya Maji kwakuwa shughuli zifanywazo na binadamu kando ya Vyanzo hivyo hupelekea mito hiyo kukauka.

hayo yamebainishwa leo na Waziri Makamba alipofanya ziara ya kikazi Kihansi Wilayani Kilolo kuangalia chanzo cha Mto Kihansi. Waziri Makamba kwa nyakati tofauti amefanya mazungumzo na wanakijiji wa Kijiji cha Mwantasi ambao wamefanya jitihada za dhati kuhifadhi Vyanzo vya Maji.

Waziri Makamba amewapongea na kuchangia kiasi cha shilingi laki mbili kwa vijiji vya Mwantasi kwa ajili ya Mfuko wa Mazingira wa Kijiji wenye lengo la kusimamia masuala za mazingira katika kijiji chao.

"Nawapongeza sana kwa jitihada mlizonazo ikiwa ni pamoja na kuwa na sheria ndogo ndogo za kutunza mazingira, nami nawaunga mkono kwa kuchangia kiasi cha shilingi laki moja kwa kijiji cha Mwantasi na laki moja kwa kijiji cha Wangama ili kuimarisha mfuko huo" Makamba alisisitiza.

Aidha Waziri Makamba amemuagiza Mkurugenzi wa Kilolo kuhakikisha fani zinazotozwa za uharibifu wa mazingira sehemu ya pesa hizo zinapelekwa katika vijiji husika ili kukuza mfuko huo na kuwaagiza wajumbe wa Kamati za Mazingira ngazi ya kijiji kuzitunza fedha hizo benki na kuagiza matumizi sahihi.

Waziri Makamba anaendelea na ziara ya kikazi katika Mikoa mbalimbali hapa nchini na leo yuko katika Mkoa wa Morogoro ambapo ametembelea Mto Kihansi na Ruaha Mkuu.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.