Habari za Punde

MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU AHANI MSIBA WA MASABURI LEO

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitia saini kwenye kitabu cha maombelezo cha marehemu Dk. Didas Masaburi nyumbani kwa marehemu Tabata Segerea,jijini Dar es salaam.Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwapa pole ndugu marehemu Dk. Didas Masaburi mapema leo Chanika,jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimpa pole Bw. Deogras Didas Masaburi (Ojambi) ambaye ni mtoto wa Marehemu Dk. Didas Masaburi na Diwani wa kata ya Chanika,jijini Dar es salaam. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Profesa Philemon Sarungi mara baada ya kukutana kwenye msiba wa Marehemu Dk. Didas Masaburi mapema leo Chanika,jijini Dar es salaam. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimpa pole na kumfariji Bi.Janeth Masaburi ambaye ni mke wa Marehemu Dk. Didas Masaburi na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) nyumbani kwa marehemu Tabata Segerea,jijini Dar es salaam. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (wa pili kushoto) pamoja na viongozi wengine wa Chama Cha Mapinduzi wakimpa pole na kumfariji Bi.Janeth Masaburi ambaye ni mke wa Marehemu Dk. Didas Masaburi na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) nyumbani kwa marehemu Tabata Segerea,jijini Dar es salaam.
 

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.