Habari za Punde

MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA CUBA AWASILI NCHINI

 Ndege ya Kampuni ya SOUTH AFRICAN iliyombeba Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Cuba Mhe. Salvador Valdes Mesa ikiwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere (JNIA) jana Jijini Dar es Salaam. Makamu huyo wa Rais yupo nchi kwa ziara ya itakayomalizika terehe 04 Septemba, siku ya Jumanne.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Cuba Mhe. Salvador Valdes Mesa akishuka katika Ndege mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere (JNIA) jana Jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Hassan Suluhu akimwongoza mgeni wake Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Cuba Mhe. Salvador Valdes Mesa mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere (JNIA) jana Jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Cuba Mhe. Salvador Valdes Mesa Aakitembelea vikundi mbalimbali vya sanaa vilivyokuwepo uwanjani kwa ajili ya kumkaribisha mara baada ya kuwasilii katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere (JNIA) jana Jijini Dar es Salaam.Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda.
Picha na Frank Shija, MAELEZO.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.