Habari za Punde

MANJI ATANGAZA KUAHIRISHWA KWA MKUTANO MKUU WA DHARULA WA YANGA KESHO

Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manjia ametangaza na kuwaomba radhi wanachama wa Yanga kwa kuahirisha mkutano Mkuu wa Dharula uliokuwa ufanyike kesho pale Makao Makuu ya Klabu hiyo Jangwani.

Manji amesema kuwa wamefikia maamuzi hayo kutokana na kupokea barua ya zuio la kufanya mkutano huo ilikupisha Mahakama kufanya taratibu zake baada ya kupokea shauri la zuio la mkutano huo kutoka kwa aliyewahi kuwa Mwanasheria wa Klabu hiyo.

Aidha Manji amewataka radhi wanachama wa Yanga kwa usumbufu wowote utakaojitokeza na hasa wale waliotoka mikoani na wale waliosafarini kuja jijini Dar kwa ajili ya kuhudhuria mkutano huo ambao wengine hutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania na Visiwani Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.