Habari za Punde

MASHABIKI KUAMUA NANI MKALI KATI YA ISHA MASHAUZI, LEYLA RASHID OKTOBA 22 DAR LIVE

WAIMBAJI wawili wanaokimbiza kwenye soko la taarab kwa hivi sasa Isha Mashauzi na Leyla Rashid wanatarajia kupanda jukwaani Oktoba 22 kuchuana na kuwadhihirishia mashabiki kuwa ni nani mkali kati yao katika miondoko ya muziki wa Taarab.

Mpambano huo wa Malkia wawili unatarajia kufanyika ndani ya ukumbi wa Dar Live Mbagala, 
ambapo Isha Mashauzi atathibitsha kuwa yeye ni malkia wa masauti matamu huku Leyla akitaka kudhihirisha kwamba yeye ndiye malkia wa taarab.
Akizungumza na mtandao huu, Mratibu wa onyesho hilo,  Hajji Mabovu alisema kuwa mpambano huo unatarajiwa kusindikizwa na bendi mbili kubwa za taarab, Jahazi Modern Taarab na Mashauzi Classic.

Wasanii hao tayari wamekwisha thibitisha makubaliano ya kufanya onesho hilo la pamoja na kusema kuwa wamefikia makubaliano hayo kwa lengo la kumaliza ubishi baina yao ambao umekuwa miongoni mwa mashabiki wa muziki huo kwa siku nyingi.

Aidha wakizungumza na mtandao huu kwa nyakati tofauti,wasani hao walitambiana huku kila mmoja akijinadi kumgalagaza mwenzake siku hiyo.

Kwa upande wa Leyla Rashid alisema kuwa kutokana na vitu vikali alivyonavyo kwa sasa, anamsikitikia mwenzake Isha Mashauzi kwa kukubali kushiriki mpambano huo kwani anaamini baada ya mpambano huo, hatoweza kupanda jukwaani kwa wiki kadhaa akijipanga kurudi kivingine.

Naye 
Isha Mashauzi ametamba kumaliza ngebe za mpinzani wake na kuwataka mashabiki kutangaza wenyewe baada ya kuona shoo hiyo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.