Habari za Punde

MAWAZIRI WA FEDHA WAJADILI NAMNA YA KUPAMBANA NA UTAPIAMLO NA UDUMAVU WA AKILI WA WATOTO

 Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim akimpogeza Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango, baada ya kuwasilisha hotuba kwa niaba ya Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan katika mkutano huo kuhusu watoto kupata lishe bora wakati wa kuzaliwa na kusisitiza wakinamama wanyonyeshe watoto ipasavyo ili kuondokana na tatizo kubwa la utapiamlo ambalo mara nyingi huwakumba watoto wanapokuwa wadogo na kusababisha kupoteza nguvu kazi ya Taifa, Jijini Washington DC.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, wa kwanza kushoto akisikiliza kwa makini hotuba ya Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim, katika mkutano uliowahusisha Mawaziri wa Fedha kutoka nchi kadhaa duniani kama vile Cameroon, Ethiophia, Senegal na Indonesia ambapo rais huyo aliwataka mawaziri hao wasimamie rasilimali fedha vizuri  hasa katika suala la kukabiliana na changamoto ya utapiamlo na udumavu wa akili kwa watoto waliochini ya umri wa miaka mitano, mkutano uliofanyika Jijini Washington DC, Marekani.
 Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim akiwa na Mawaziri wa Fedha wa Afrika akiwemo na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Philiph Mpango(wa nne kutoka kulia),Jijini Washington DC. 
7820- Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akiwasilisha hotuba kuhusu ni jinsi gani Tanzania imejipanga kukabiliana na tatizo la utapiamlo na udumavu wa akili kwa watoto walio na umri wa chini ya miaka mitano, alipomuwakilisha Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Jijini Washington DC, Marekani.
 Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim akiwa na Mawaziri wa Fedha wa Afrika akiwemo na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Philiph Mpango(wa nne kutoka kulia),Jijini Washington DC.
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akiwasilisha hotuba kuhusu ni jinsi gani Tanzania imejipanga kukabiliana na tatizo la utapiamlo na udumavu wa akili kwa watoto walio na umri wa chini ya miaka mitano, alipomuwakilisha Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Jijini Washington DC, Marekani. 

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.