Habari za Punde

MERCK KUTOA MSAADA WA TEMBE MILIIONI 500 AFRIKA

Kutoka Abidjan, Ivory Coast, Oktoba 19, 2016 – 
·        Zaidi ya watu milioni 100, hususani watoto, wametibiwa ugonjwa wa kichocho tangu 2007
  • Kwa mara ya kwanza Merck kutoa takriban tembe milioni 10 kwa Shirika la Afya Duniani (WHO) nchini Ivory Coast.

Merck (MerckGroup.com), kampuni kubwa ya sayansi na teknolojia, imetangaza leo kuwa imetoa msaada wa tembe milioni 500 za kutibu ugonjwa wa minyoo ya kichocho unaodhuru kwa siri kwa Shirika la Afya Duniani (WHO). Katika shule inayopatikana takriban kilomita 25 magharibi kaskazini mwa Abidjan, wawakilishi kutoka Merck, WHO na Wizara ya Afya ya Ivory Coast wametangaza kwa sauti moja uzinduzi wa usambazaji wa dawa hiyo nchini Ivory Coast.

Juhudi za Merck za kupambana na ugonjwa wa kichocho zilianza mwaka 2007 na zinahusisha nchi 35 barani Afrika. Zaidi ya wagonjwa milioni 100, hususan watoto wa shule, wametibiwa hadi leo hii. “Tumejizatiti kuendelea kutoa tembe milioni 250 kila mwaka hadi ugonjwa huu mbaya uishe,” alisema Belén Garijo, mwanabodi wa Bodi ya Utendaji ya Merck na Mkurugenzi Mtendaji wa Huduma ya Afya. “Kutoa msaada wa tembe milioni 500 za praziquantel leo hii kunaonyesha hatua kubwa tuliyoipiga katika kufanikisha lengo hili.” Garijo aliongezea.

Katika sherehe iliyofanyika katika shule ya msingi ya kijiji cha Attinguie, wawakilishi wa Wizara ya Afya Ivory Coast na British Schistosomiasis Control Initiative (SCI) walisimamia tembe za praziquantel za matibabu ya ugonjwa wa kichocho kwa watoto. Watoto hupokea kati ya tembe moja hadi tano, kulingana na urefu wao. Pia, walimu waliwaelezea sababu za ugonjwa wa minyoo ya kitropiki. Kwa lengo hili, Merck imetoa msaada wa jumla ya vijitabu 20,000 vya kuelimisha kwa WHO kwa ajili ya Ivory Coast.

Kwa mujibu wa WHO, zaidi ya asilimia 20 ya idadi ya watu nchini Ivory Coast wanahitaji matibabu. Hadi leo, shirika la maendeleo la Marekani USAID pamoja na Schistosomiasis Control Initiative (SCI) wameiunga mkono serikali ya Ivory Coast katika vita dhidi ya ugonjwa wa kichocho. Kama mwanachama wa Global Schistosomiasis Alliance, Merck imekuwa ikishirikiana na mashirika yote mawili tangu 2014. Ndani ya ushirikiano huu, kampuni hii imetoa msaada wa tembe milioni 3.6  kwa WHO kwa mwaka 2016. Kwa sababu hiyo, Ivory Coast imenufaika kwa mara ya kwanza kutokana na ushirika kati ya Merck na WHO. Mwaka wa 2017, Merck itatoa tembe milioni 6.5 kwa WHO kwa ajili ya nchi ya Afrika Magharibi.

Ugonjwa wa kichocho unaathiri takriban watu milioni 260 duniani kote. Kiwango cha maambukizi kipo juu zaidi kwa watoto, na madhara yake ni makubwa zaidi. Ugonjwa huu wa vimelea unaathiri ukuaji, husababisha ulemavu wa kujifunza, na husababisha upungufu wa damu mwilini. Merck inatoa msaada wa tembe za praziquantel kwa WHO kama sehemu ya uwajibikaji wake katika jumuiya na ndani ya Afya, mojawapo ya shughuli zake za mkakati wa uwajibikaji wa shirika. Praziquantel ni matibabu bora yanayovumiliwa na yenye ufanisi zaidi kufikia sasa kwa ugonjwa wa kichocho. Aidha, Merck inatoa usaidizi wa mipango ya kielimu na programu za kuhamasisha, kufanya utafiti wa tiba ya ugonjwa wa kichocho kwa kila watoto wachanga na kushirikiana na washirika katika Umoja wa Kupambana na Kichocho Duniani (Global Schistosomiasis Alliance).

Distributed by APO on behalf of Merck.
Vyombo vya habari Mawasiliano:
Friederike Segeberg    
+49 6151 72-4081


Kichocho:
Kichocho ni hali sugu na ni mojawapo ya magonjwa mabaya zaidi ya kawaida na yanayoletwa na vimelea katika nchi za kitropiki. Inakadiriwa kuwa watu milioni 260 wameambukizwa duniani kote na akriban watu 200, 000 wanapoteza maisha kila mwaka kutokana na ugonjwa huo. Ugonjwa huo sugu unasambazwa na minyoo bapa. Umeenea zaidi katika maeneo ya kitropiki na yale yanayopakana na tropiki ambapo sehemu kubwa ya idadi ya watu hawapati maji safi na vifaa vya usafi. Watu wanaambukizwa ugonjwa huu kupitia mabuu ya minyoo hasa kwenye maji baridi, kwa mfano wanapofanya kazi, kuogelea, kuvua samaki au kufua nguo. Mabuu hayo yasiyowezakuonekana hupenyeza kwenye ngozi ya binadamu, na kuingia katika mishipa ya damu na kushambulia viungo vya ndani. Kiwango cha maambukizi kipo juu zaidi miongoni kwa watoto wa shule. Praziquantel ndicho kiambato amilifu ambacho kinatibu aina zote za ugonjwa wa kichocho. Kwa hivyo, WHO imeonyesha praziquantel, kuwa suluhisho nafuu zaidi kwa afya ya wagonjwa wahitaji, kama dawa ya chaguo lao.

Programu ya Msaada wa Praziquantel ya Merck:
Merck ilianzisha Programu ya Msaada wa Praziquantel kwa ushirikiano na WHO mwaka 2007. Tangu hapo, zaidi ya tembe milioni 500 zimetolewa na zaidi ya wagonjwa milioni 100 wametibiwa, hasa watoto wa shule. Merck imejitolea kuimarisha juhudi zake katika kupambana na  ugonjwa huu wa kitropiki hadi kichocho kiishe. Hadi sasa, Merck inatoa msaada kwa WHO wa hadi tembe milioni 250 kila mwaka . msaada uliopangwa wa kila mwaka una thamani ya takribani milioni $23 za Marekani. Aidha, Merck inaunga mkono programs za uhamasishaji shuleni barani Afrika ili kuelimisha watoto kuhusu sababu za ugonjwa wa kichocho na njia za kuuzuia. Pia, kama sehemu ya ushirikiano kati ya sekta za umma na sekta binafsi, kampuni hii inafanya utafiti wa uundaji mpya wa praziquantel ambao pia unaweza kutumika kwa watoto wachanga zaidi. Hadi sasa, tembe hizo ni nzuri tu kwa watoto walio na zaidi ya umri wa miaka sita. Mwishoni mwa mwaka 2014, Merck ilizindua Umoja wa Kupambana na Kichocho Duniani (Global Schistosomiasis Alliance) pamoja na washirika kama vile Bill & Melinda Gates Foundation, shirika la Misaada la Marekani USAID, Schistosomiasis Control Initiative (SCI) pamoja na World Vision International.
Maelezo zaidi kuhusu vita dhidi ya ugonjwa wa kichocho yanapatikana Mtandaoni (http://APO.af/vB2EJY).

Kuhusu Merck:
Merck ni kampuni ya sayansi na teknolojia inayoongoza katika huduma ya afya, sayansi ya maisha na nyenzo za utendakazi. Takriban, waajiriwa 50,000 wanafanya kazi ili kuendeleza zaidi teknolojia zinazoboresha na kuimarisha maisha - kuanzia tiba za dawa za kibiolojia ili kutibu saratani na uzulufu anuwai, mifumo ya kisasa kwa ajili ya utafiti na uzalishaji wa kisayansi, hadi mwonekano bora zaidi wa simu za kisasa na televisheni za LCD. Mwaka 2015, Merck ilizalisha mauzo ya bilioni € 12.85 katika nchi 66.
Ilianzishwa mwaka 1668, Merck ndiyo kampuni ya zamani zaidi ya dawa na kemikali ulimwenguni. Familia ya watangulizi inaendelea kuwa mmiliki mkuu wa kikundi cha mashirika yaliyoorodheshwa kwa umma. Kampuni hii inahifadhi haki za ulimwengu kwa jina na chapa ya Merck. Isipokuwa kwa Marekani na Kanada pekee, ambapo kampuni huendeshwa kama MD Serono, MilliporeSigma na EMD Performance Materials.

Matoleo yote ya habari za Merck yatasambazwa kupitia barua pepe wakati uo huo yanapatikana kwenye tovuti ya Merck. Tafadhali tembelea www.merckgroup.com/subscribe ili kujisajili mtandaoni, kubadilisha uteuzi wako au kusitisha huduma hii.
SOURCE 
Merck

Multimedia content

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.