Habari za Punde

MJADALA WA MUSWADA WA SHERIA YA HUDUMA ZA HABARI WAENDELEO MJINI DODOMA CHINI YA KAMATI YA HUDUMA NA MAENDELEO YA JAMII

Na Mwandishi Wetu Dodoma
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii leo imekutana Mnini Dodoma na kuendelea na kuujadili Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari kwa kuendelea kupitia kifungu kwa kifungu katika Muswada huo.

Akifungua kikao hicho Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Peter Serukamba alisema wamekutana katika kikao hicho ikiwa ni muendelezo wa kupitia Muswada huo kwa makini kabla ya kupelekwa Bungeni kwa ajili ya kujadiliwa na wabunge.

Aliongeza kuwa ni wakati kwa wajumbe kuendela kuujadili kutoa maoni yao katika kuuboresha Muswaada huo ili waweze kupeleka Muswada ambao utaleta Sheria iliyo bora kwa manufaa ya tasnia ya habari na watanzania kwa ujumla.

“Wajumbe nawaomba tuujadili na kuuchambua Muswada huu kwa makini sana kwani sisi ndio watungaji wa Sheria na tutoe maoni na marekebisho yatakaoufanya Muswada huu kutoa Sheria iliyo bora” alisisitiza Mhe. Serukamba.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii inaendelea kupokea maoni kutoka kwa wadau habari  kuhusu Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari kupitia barua pepe ya cna@bunge.go.tz.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.