Habari za Punde

MKUU WA MKOA DAR, PAUL MAKONDA ATANGAZA KUTOA SH. MILIONI 10 KUMSAIDIA KIJANA SAID ALIYETOBOLEWA MACHO
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam , Paul Makonda akiwa na Said Ally, Kijana aliyetobolewa macho, wakati Mkuu wa Mkoa alipozungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini leo.

Mkuu wa Mkoa Dar, Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari.

Mkuu wa Mkoa Paul Makonda akiwa na Kijana Said Ally na Mke wa kijana huyo, Zara Sudi mara baada ya mkutano na waandish wa Habari.

**************************

Na Ripota wa Mafoto Blog, Dar
Siku chache baada ya kukamatwa mtuhumiwa aliyedaiwa kumtoboa macho kijana Said Ally mkazi wa Buguruni kwa Mnyamani, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam , Paul Makonda ametangaza kuendelea kumsaidia kijana huyo katika hatua zake zote za matibabu na kuahidi kumpatia mtaji wa Shilingi Milioni kumi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Makonda alisema kuwa mara baada ya kufanyika uchunguzi na madaktari Bingwa wa Muhimbili imeogundulika kuwa kijana Said, hatoweza kupata tena uwezo wa zaidi ya kuhitaji matibabu ya ziada.
KUSOMA ZAIDI BOFYA READ MORE
Aidha Mhe.Makonda alisema kuwa Serikali imejitolea kumsaidia usafiri kijana huyo kwa kipindi chote ili aweze kufanikisha shughuli zake za matibabu.

“Serikali ya mkoa imetoa gari ambayo atatumia kwa kipindi chote akiwa anaenda kupatiwa matibabu na shughuli zingine ambazo atakuwa anafanya mpaka hapo atakapokuwa sawa”alisema Makonda.

Kwa upande wake Kijana Said Ally,  aliishukuru Serikali na madaktari kwa jitihada walizozionesha na wanazoendelea kuzionyesha juu yake pamoja na Clouds Media kwa kujitolea kuutangazia Umma kuhusu ukatili huo.

“Kiukweli namshukuru sana Mungu kwa msaada ninaondelea kupata kutoka kwa mkuu wa Mkoa na Serikali kwa ujumla, Clouds na madakatari wote naomba mungu aweze kuwapa maisha marefu na moyo wa kijitoa kama wafanyavyo” alisema Said.

Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda alimaliza kwa kusema kuwa Serikali ya mkoa inandaa utaratibu kwa ajili ya watu wengine ambao wanahitaji kujitolea kumsaidia Said hivyo jumatatu atatangaza rasmi.
Kijana Said Mrisho anayedaiwa kujeruhiwa na kutobolewa macho na Salumu Henjelewe maarufu kama Scorpion (katikati), akisaidiwa na ndugu zake wakati akiingia ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaa, Paul Makonda kuzungumza na waandishi wa habari.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kabla ya kumpa fursa kijana Said kuzungumza na wanahabari.
Kijana Said Mrisho (kulia), akizungumza na wanahabari. Kulia kwake ni mke wake Stara Soud.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam akiwa ameinama kwa uchungu wakati kijana huyo alipokuwa akizungumza na wanahabari.
Kijana Said Mrisho anayedaiwa kujeruhiwa na kutobolewa macho na Salumu Henjelewe maarufu kama Scorpion (kulia), akilia kwa uchungu wakati akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda leo. Kushoto ni mke wake, Stara Soud.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Grace Magembe (kushoto), akimfariji kijana Said Mrisho.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akimfariji kijana Said Mrisho.
Mama yake Said Mrisho, Halima Lwiza Abdallah akilia.
Ndugu zake Said Mrisho wakitoka ofisi ya mkuu wa mkoa Dar es Salaam baada ya kuzungumza na wanahabari. Kushoto mbele ni mama yake Said, Halima Lwiza Abdallah na kulia ni mke wake, Stara Soud.
Said Mrisho akisaidiwa kushuka ngazi wakati akitoka kuzungumza na wanahabari ofisi ya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam
.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.