Habari za Punde

MNYAMA SIMBA AWAZUIA WAKATA MBAO KUTOKA NA MZIGO WA MBAO MSITUNI UHURU, 1-0

TIMU ya Simba ya jijini Dar es Salaam, leo tena imeweza kuendeleza wimbi la ushindi katika mechi zake za Ligi Kuu Bara baada ya kuwazuia wakata Mbao kutotoka na mzigo wa Mbao katika Uwanja wa Uhuru leo jioni.

Alikuwa ni Muzamil Yassin aliyewaduwaza Mbao Fc katika dakika ya 87, na kuwainua mashabiki wa Simba vitini zikiwazimebakia dakika tatu mpira kumalizika na kuzima matumaini ya wakata mbao hao waliokuwa wakijipa moyo kuwa wanakaribia kuvuka pori lenye mnyama mkali msituni na mzigo wao wa Mbao.

Kwa ushindi huo wa bao 1-0 Simba SC inaendelea kubaki kileleni kuongoza usukani wa Ligi Kuu bara wakiwa na jumla ya Pointi 26 baada ya kucheza jumla ya ichezo 10 ikishinda mechi nane na kutoa sare mechi mbili.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.