Habari za Punde

MPAMBANO WA ISHA MASHAUZI, MALKIA LEYLA ULIVYOBAMBA DAR LIVE


Baada ya Isha kuanza kukamua shabiki huyu alikunwa na hivyo kuvamia jukwaa kwenda kumtuza.
Leyla akifanya yake baada kupanda jukwaani.
*****************************************
MASHABIKI wa burudani, hususan muziki wa taarab, usiku wa kuamkia jana walipata burudani ya aina yake wakati wakali wa muziki huo, Isha Mashauzi na kundi lake la Mashauzi Classic kwa upande mmoja na Leyla Rashid kwa upande mwingine akiwa na kundi lake la Jahazi Modern Taarab, walipotoana kijasho kwenye onesho maalum la kutaka kujua nani mkali kati yao.

Kabla ya mpambano huo kulikuwa na ubishani mkali kwa mashabiki ambapo upande fulani ulisema Isha ndiye mkali kuliko Leyla huku wengine wakisema “aaah, wapi bwana Leyla ndiyo mkali zaidi; pale Isha haingii hata kwa nini”

Hatma ya ubishi huo ni mpambano uliowakutanisha wawili hao na kuwaacha mashabiki wakijionea na kuamua wenyewe. 

Kabla ya wakali hao kupanda jukwaani mshereheshaji wa shughuli hiyo, Aisha Mbegu, wa Redio Times ilibidi arushe sarafu hewani ili kumpata mwanamuziki wa kuanza kulivamia jukwaa maana walianza kutegeana. Baada ya sarafu kurushwa Isha ndiye aliyeangukiwa na zali la kuanza kuonesha mavitu vyake jukwaani.
Sehemu ya umati uliofurika ukumbini hapo kufuatilia mpambano huo.
Leyla akiwanogesha mashabiki. Picha/Habari na Richard Bukosi (GPL)

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.