Habari za Punde

MTANGAZAJI PAUL JAMES 'PJ' KUBURUZWA MAHAKAMANI NA EFM REDIO

Mtangazaji maarufu aliyewahi kutangaza kituo cha redio cha Clouds Fm nakujiunga na EFM redio na baadaye kurudi tena Clouds Fm amefunguliwa mashtaka katika mahakama ya kazi jijini Dar es salaam na EFM redio kwa kile kinachodaiwa kuwa amekiuka mkataba wa kazi wa kituo hicho.

Kufuatia mashtaka hayo, Efm inadai fidia ya shilingi milioni 200 kwa mtangazaji huyo ambaye alijiunga na kituo hicho kutoka clouds fm na baadae kudaiwa kukatisha mkataba kiholela na kurudi tena clouds fm bila kufuata makubaliano pamoja na sheria alizokubaliana nazo katika mkataba wake awali wakati alipojiunga na efm redio.

Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa tarehe 23/11/2016 katika mahakama ya kazi Jijini Dar es salaam.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.