Habari za Punde

MVUA YANYESHA UWANJA WA UHURU DAR, MBAO 'NGUMU' ZAROWA 3-0

 Shabiki wa Yanga akishangilia huku akionesha ishara ya Msumeno kukata baada ya bao la tatu.
 Kocha wa Yanga akiwasisitiza wachezaji wake kwa kuwahamasisha, Ni kama anasema 'Kata hizo Mbaoooooooo'......
Amis Tambwe akikosa bao katika kipindi cha kwanza baada ya kipa wa Mbao kutokea.
 Kipindi cha pili Amis Tambwe apata bao
 Amis Tambwe akishangilia baolake
************************************************
'YANGA YAZIDI KUFUKUZA MWIZI KIMYA KIMYA'
Na Ripota wa Mafoto Blog, Dar
MABINGWA watetezi wa ligi kuu Bara, Yanga SC leo wameibuka na ushindi wa mbao 3-0 dshidi ya Mbao Fc ya jijini Mwanza na kufikisha jumla ya Pointi 27 nyuma ya Watani wao za Jadi Simba weye jumla ya Pointi 32.

Zikionekana kusomana mchezo kipindi cha kwanza kilikuwa kigumu kwa timu zote mbili huku Yanga wakijaribu kufanya mashambulizi ya kushitukiza baada ya ukuta wa Mbao Fc kuonekana kuwa makini zaidi katika kuhakikisha hawaruhusu goli la mapema na hadi timu hizo zinakwenda mapumziko zilikuwa bado sare ya 0-0.

Kipindi cha Pili kilianza kwa kasi kwa Yanga kutafuta goli na katika dakika ya 53, beki wa Yanga Viceny Bosou, aliunganisha mpira wa adhabu ndogo uliopigwa na Kiungo Haruna Niyonzimana kumshinda golikipa wa Mbao na kutinga wavuni.

Bao la pili lilifungwa na Mbuyu Twite katika dakika ya 55, aliyerusha mpira ulioguswa na Kipa wa Mbao  Emanuel Mseja na kisha kutinga wavuni na kuandika bao la pili  na kuingia nyavuni na kuiandikia Yanga goli la pili.

Amisi Tambwe akitumia madhaifu ya mabeki hao anaiandikia Yanga goli la tatu na la ushindi.

Mabadiliko ya Yanga yalifanya safu ya ulinzi ya Mbao kuanza kucheza kwa umakini zaidi hasa baada ya kuingia Donald Ngoma na kutoka Obrey Chirwa, Deus Kaseke kutoka na kuingia Juma Mahadhi pamoja na Hassan Kessy na nafasi yake kuchukuliwa na Kiungo Thaban Kamusoko.

Baada ya ushindi huo, Yanga wanakwea pipa hadi Jijini Mbeya kwenda kuvaana na Mbeya City Novemba 02, na kumaliza na Prison Novemba 06  kabla ya kurejea tena Dar es salaam kuvaana na Ruvu Shooting Novemba 11.
 Deus Kaseke akichuana kuwania mpira na Youssouf Ndikumana.
 Kiungo wa Yanga, Haruna Niyonzima, akiwania mpira na beki wa Mbao Fc, David Majinge.
 Mshike mshike ulikuwa ni kati ya Beki wa Mbao Fc, Steve Mganya (kushoto) na Kiungo wa yanga, Simon Msuva, ...cheki hapa......
 Hii ni Robaaaaa, Shaulin Tample ama veepeeeee......
 Mashabiki wakiwa na mabango yenye ujumbe ........
 Beki wa Mbao Fc, Asante Kwasi, akimdhibiti mshambuliaji wa Yanga,Amis Tambwe.....
 Shabiki wa Yanga akikatika jukwaani akiwa na msumeno mara baada ya kufungwa bao la tatu.
Kocha wa Yanga Hans Pluijm, akiangalia muda baada ya baola tatu.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.