Habari za Punde

MWAMKO MDOGO WA USHIRIKI WA WANANCHI SIKU YA USAFI KITAIFA MKOANI MOROGORO

Kaimu Mkurugenzi Idara ya Mazingira Bwana Richard Muyungi akiwa katika Manispaa ya Morogoro kata ya Kihonda, akishiriki kufanya usafi katika siku ya jumamosi ya mwisho wa mwezi ambayo ni siku ya usafi kwa Tanzania nzima.
Sehemu ndoogo ya idadi ya Wananchi wa Manispaa ya Morogoro waliojitokeza kushiriki katika siku ya usafi wa mazingira ya kila jumamosi ya mwisho wa mwezi iliyofanyika katika kata ya Kihonda. Wananchi wengi wamelalamika kutokuwa na elimu juu ya siku hiyo ya usafi.
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Mazingira Bwana Richard Muyungi akiwa katika Manispaa ya Morogoro kata ya Kihonda, akishiriki kufanya usafi katika siku ya jumamosi ya mwisho wa mwezi ambayo ni siku ya usafi kwa Tanzania nzima.
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Mazingira Bwana Richard Muyungi akitoa maagizo juu ya kuhamasisha Wananchi juu ya kushiriki katika siku ya usafi juamosi ya mwisho wa mwezi, kwa Afisa Afya wa Mkoa wa Morogoro Bwana Simon Malulu na Afisa Afya na Mazimgira wa Wilaya Bwana Amri Ugumba.
************************************
Serikali ya Mkoa wa Morogoro imeagizwa kufuata maagizo ya Serikali kuwa kila jumamosi ya mwisho wa mwezi kuwa ni siku ya kufanya usafi wa mazingira. Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais, Richard Muyungi aliposhiriki kufanya usafi wa siku ya jumamosi ya mwisho wa mwezi katika Manispaa ya Morogoro.

Tukio hilo limehudhuriwa na Watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Manispaa ya Morogoro na idadi ndogo sana ya Wananchi. Akiongea katika eneo la tukio mkurugenzi Muyungi amesema kuwa amesikitishwa sana na Wananchi kutokuwa na elimu ya kushiriki katika swala zima la usafi wa mazingira na wala kutokuonyesha kuwa na uelewa wowote juu ya siku ya usafi Kitaifa.

‘Kwa kweli nimesikitishwa sana na hali hii nilioona leo Wananchi hawana uelewa kabisa juu ya suala zima la siku ya usafi na wala hawajui nini kinachoendelea juu ya usafi’ alisema Muyungi. Mkoa wa Morogoro bado upo nyuma sana kwenye kuzingatia siku ya usafi na haya elimu ya usafi kwa wananchi wake bado haijawaingia.

Wakiongea mbele ya Bwana Muyungi, Afisa Afya wa Mkoa Bwana Simon Malulu na Afisa Afya na Mazingira wa Manispaa Bwana Amri Ugumba wamekiri kuwa mwamko wa ufanyaji wa usafi kwa siku hii ya leo ni mdogo san. Wananchi bado hawana uelewa mkubwa juu ya siku hiyo. Wameahidi kuanza kufanyia kazi suala hilo na pia kuanza kuchukua hatua kwa wote watakaopuuzia siku ya usafi ambayo ni juamosi ya mwisho wa mwezi.

Ofisi ya Makamu Rais ni MRatibu wa masuala yote ya Mazingira hivyo basi hutembelea na kufuatilia kwa ukaribu kujua Mikoa mbalimbali wanavyosimamia masuala ya utunzaji wa mazingira na usafi kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.