Habari za Punde

NAIBU WAZIRI STELLAH MANYANYA AWAONYA WAKANDARASI UJENZI NYAKATO NA IHUNGO


 Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali (Mst) Salum Kijuu akimueleza Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. Mhandisi Stella Manyanya hatua zinazoendelea kuchukuliwa na serikali katika kurudisha hali baada ya tetemeko la ardhi kutokea mkoani huko.
Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. Mhandisi Stella Manyanya na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali (Mst) Salum Kijuu wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Wizara ya Elimu na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera.
Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. Mhandisi Stella Manyanya akikagua vifaa ndani ya maabara katika shule ya sekondari ya Ihungo ambayo pia iliathiriwa kiasi kikubwa na tetemeko la ardhi lililotokea mkoani kagera mapema mwezi September 2016. KUSOMA ZAIDI BOFYA READ MORE

Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. Mhandisi Stella Manyanya akiongea na baadhi ya wafanyakazi waliopo katika eneo la ujenzi mpya wa shule ya sekondari ya Ihungo na kuwataka kufanya kazi kwa viwango stahiki na kwa wakati pamoja na wakijiepusha na vitendo vya wizi wa vifaa vya ujenzi.
Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. Mhandisi Stella Manyanya akioneshwa baadhi ya majengo yatayojengwa upya katika shule ya sekondari ya Nyakato ambayo pia baadhi ya majengo yake yaliathiriwa na tetemeko la ardhi hiyo kuifanya kuamuliwa kujengwa upya
 Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. Mhandisi Stella Manyanya akimuonesha jambo mwanafunzi mwenye ulemavu katika shule ya msingi Mgeza Mseto iliyopo mkoani kagera alipoitembelea kuona namna ilivyoathiriwa na tetemeko la ardhi kwenye baadhi ya majengo yake.
 Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. Mhandisi Stella Manyanya akiwaeleza jambo watoto wenye ulemavu wa ngozi (ALBINISM) wa shule ya Msingi ya Mgeza Mseto iliyopo mkoani kagera alipoitembelea kuona namna ilivyoathiriwa na tetemeko la ardhi kwenye baadhi ya majengo yake.
 Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. Mhandisi Stella Manyanya akiwaeleza jambo watoto wenye ulemavu wa ngozi (ALBINISM) wa shule ya Msingi ya Mgeza Mseto iliyopo mkoani kagera alipoitembelea kuona namna ilivyoathiriwa na tetemeko la ardhi kwenye baadhi ya majengo yake.
 Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. Mhandisi Stella Manyanya akiongea na wanafunzi wa Shule ya Msingi Mgeza Mseto iliyopo mkoani kagera alipoitembelea kuona namna ilivyoathiriwa na tetemeko la ardhi kwenye baadhi ya majengo yake. PICHA NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO
********************************************
Na Benedict Liwenga-MAELEZO
Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. Mhandisi Stella Manyanya leo amewasili Mkoani Kagera na kutembelea miundombinu ya sekta ya elimu ili kujionea namna serikali inavyorejesha hali kama awali kutokana na tetemeko la ardhi lililotokea September 10 mwaka huu.

Akiwa katika shule ya sekondari ya Ihungo, Mhandisi Manyanya amewataka wakandarasi waliopewa dhamana ya kusimamia ujenzi upya wa majengo mapya ya Shule za Ihungo na Nyakato kujenga kwa kuzingatia viwango sahihi kulingana na maelekezo ya wataalam wa miamba.

“Mmepewa dhamana ya kusimamia ujenzi upya wa shule hii, nawaombeni muzingatie viwango sahihi wakati mnajenga hasa kwa kuangalia mapendekezo ya wataalam wa miamba waliyoyatoa ili kuyaweka majengo katika hali ya usalama” Alisema Mhandishi Manyanya.

Aidha Mhandisi Manyanya amewatahadharisha wakandarasi wenye tabia ya kudokoa vifaa vya ujenzi kutothubutu kufanya hivyo kwani yeyote atayeiba vifaa hivyo atachukuliwa hatua za kisheria.

Katika kuhakikisha wanafunzi wenye ulemavu tofauti wanapata elimu sawa Mhandisi Manyanya amewataka walimu wa shule ya msingi Mgeza Mseto kutenda haki sawa wanafunzi wote bila kujali aina ya ulemavu alionao mwanafunzi.

Katika hatua nyingine Mhandisi Manyanya amezitaka shule hasa za sekondari nchini kuanzisha mashamba darasa yatakayowawezesha wanafunzi kujifunza kwa vitendo shughuli za kilimo na kusaidia kuifanya shule kuwa na hifadhi ya kutosha ya chakula.

Kwa upande wa walimu Mhandisi Manyanya amewapongeza walimu wa wilaya ya Bukoba kwa kujituma na kuwekeza katika kilimo cha migomba na kuwataka walimu kote nchini kuiga mfano huo ili kuwa na chakula cha kutosha na kujiongezea kipato cha kuendesha maisha yao ya kila siku. 

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.