Habari za Punde

SCORPION AFUTIWA MASHITAKA NA MAHAKAMA YA ILALA, KESI YAKE YAHAMISHIWA MAHAKAMA KUU.

Shauri la kesi ya jinai inayomkabili mtuhumiwa Salum Njwete almaarufu kwa jina la Scorpion,limeondolewa katika mahakama ya wilaya ya Ilala na
kuhamishiwa katika Mahakama kuu jijini Dar es Salaam, kutokana na ombi lililowasilishwa katika mahakama hiyo na wakili upande wa 
Mashtaka Munde Kalombora, na Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo Mhe. Adelf Sachore na kuridhia.
Taarifa tulizozipata kutoka Mahakama ya Ilala Jijini Dar Es Salaam, zinasema kuwa Kijana anayetuhumiwa kumtoboa macho Said ajulikanae kwa jina la Scopion Amefutiwa shitaka la unyang’anyi kwa kutumia silaha lililokuwa likimkabili.
**********************************
*Taarifa zinasema kuwa Upande wa mashtaka umeomba shitaka hilo liondolewe mahakamani kwa sababu hawana nia ya kuendelea na kesi hiyo.

Na Mwandishi Wetu, Dar
Mahakama ya Wilaya ya Ilala, imemfutia shtaka linalomkabili mshtakiwa Salumu Njwete baada ya upande wa mashtaka kuomba shtaka hilo liondolewe mahakamani kwa sababu hawana nia ya kuendelea na kesi hiyo.

Kutokana na maombi hayo, Hakimu Adelf Sachore amekubaliana na ombi hilo kwa kuzingatia kifungu namba 91 kifungu kidogo cha kwanza cha sheria ambacho kinampa Mamlaka Mkurugenzi Wa Mashtaka nchini (DPP) kuondoa shtaka mahakamani muda wowote ili mradi kama kesi hiyo haijatolewa hukumu.

Lakini kifungu hicho kinampa Mamlaka DPP kumshtaki mshtakiwa huyo endapo kama ana nia ya kuendesha shtaka hilo.

Njwete anakabiliwa na shtaka la unyang'anyi wa kutumia silaha na kumjeruhi Saidi Mrisho. Lakini shtaka hili limefutwa hata hivyo anaweza kufunguliwa shtaka lingine.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.