Habari za Punde

*SIMBA WAIGOMEA YANGA WAKIWA PUNGUFU, BAO LA TAMBWE LAZUA BALAA MASHABIKI WANG'OA VITI

 TIMU ya Simba leo imeedelea kutakata katika michezo yake baada ya kuwagomea mahasimu wao Watani wa Jadi na kulazimisha sare ya 1-1 katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa leo jioni kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Baada ya Droo hiyo Simba wamefikisha jumla ya Pointi 17 huku wenzao wa Yanga wakifikisha Pointi 11 na Usukani wa Ligi hiyo ukiendelea kushikiliwa na Simba.

Lilikuwa ni bao la Amisi Tambwe katika dakika ya 28 lililozua utata na kuzua tafrani baina ya Mwamuzi na wachezaji wa Simba na kusababisha Nahodha wa timu hiyo, Jonas Mkude kulimwa kadi Nyekundu, huku mashabiki wao wakifanya vurugu kubwa kwa kung'oa viti na kurusha uwanjani,jambo lililowafanya askari Polisi kuanza kufyatua mabomu ya machozi ili kuwatawanya mashabiki hao.
 Amisi Tambwe akijiandaa kupiga shuti na kufunga bao la kuongoza kwenye mchezo wa leo dhidi yao na Simba huku akizongwa na mabeki wawili.
 Shiza Kichuya akishangilia bao lake alilopiga kona na kutinga moja kwa kwa moja wavuni na kuisawazishia timu yake ya Simba katika dakika ya 87.
 Kipa wa Simba akiwa hoi chini huku akilalamika kwa mwamuzi baada ya kufungwa bao na Amis Tambwe.
 Mwamuzi akimlima kadi nyekundu Nahodha wa Simba Jonas Mkude baada ya kumsukuma mwamuzi akipiga bao la amis Tambwe.
Kipa wa Yanga Ally Mustafa akiokoa moja ya hatri langoni kwake.
Kamusoko akiwatoka mabeki wa Simba
Wachezaji wa Simba wakimzonga mwamjuzi
Ibrahim Ajib akichuana na Amis Tambwe
Deus Kaseke akiwania mpira na beki wa Simba, Bokungu
Bokungu akiruka kukweoa kwanja la Mwinyi Haji 
Heka heka langoni mwa Simba
Ngoma akiwania mpira na kipa wa Simba, Agban
Donald Ngoma akimtoka beki wa Simba
Sehemu ya mashabiki wa Simba
Wengine ilikuwa ni furaha kabla ya upepo kubadilika
Sehemu ya mashabiki wakiwa wamejifunika maboksi kujikinga na jua
Bango la mashabiki wa Yanga
Haikuweza kufahamika shabiki huyu wa Yanga alikuwa amepandisha mashetani ama vipi
Shabiki akipigwa na butwaa
Mashabiki wakijiselfie
Hapa Mashabiki wa Simba kimyaaaaaaa
Na hapa ni zamu yao mashabiki wa Yanga kimyaaaaa
Mashabiki wa Simba wakiwa na huzuni huku wakijificha kukwepa moshi wa mabomu ya machozi
Furaha ikahamia kwao....

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.