Habari za Punde

SIMBA WAZIDI KUJICHIMBIA KILELENI, WAWABANJUA KAGERA SUGAR 2-0

LILIKUWA ni bao la Penati la dakika ya 75 la Shiza lililopoteza matumaini ya Kagera Sugar angalau kuambulia sare dhidi yao na Simba iliyoendeleza ubabe katika Ligi Kuu Bara kwa kuzidi kujichimbia kileleni kwa ushindi wa mabao 2-0 katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Uhuru jioni ya leo.

Bao la kwanza lilifungwa na 
Muzamil Yassin katika dakika ya 44 akimalizia kazi nzuri ya 
Shizza Kichuya aliyefikisha jumla ya mabao saba katika msimamo wa wafungaji bora katika Ligi Kuu Bara.

Kwa ushindi huo sasa Simba wanafikisha jumla ya Pointi 23,
baada ya kushuka dimbani mara tisa. 

MATOKEO MENGINE YA MECHI ZA LEO:
SIMBA     2 – KAGERA 0
STAND UNITED  1 – AFRICAN LYON  1
JKT RUVU     1 -- MWADUI FC 1

MSIMAMO WA LIGI KUU BARA

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.