Habari za Punde

SIMBA YA 'MWENDO KASI' YAENDELEA NA KASI YA KUJIIMARISHA KUTWAA UBINGWA

MPAKA sasa Haijapoteza mchezo ikiendelea kuibuka na ushindi katika mechi zake inazoendelea kucheza na kujikusanyia Pointizinazoendela kuwaweka kileleni mwa Ligi Kuu Bara huku wakiwa namatumainiiibaoya kutwaa Kombe laLigi Kuu msimu huu.

Ushindi wa leo wa mabao 3-0 dhidi ya Toto African umeiwezesha Simba kujikusanyia jumlaya pointi 29 baada ya kucheza mechi 11 huku wakifuatiwa na mahasimu wao Yanga walio nafasi ya pili wakiwa na jumlaya pointi 21.

Katika mchezo huo mabao yalifungwa na Muzamil Yassin katika dakika ya 42 akimalizia pasi ya Frederick Blagnon.

Hatimaye alikuwa ni Laudit Mavugo aliyeingia kuchukua nafasi ya Blagnon aliyeumia na kuandika bao la pili katika dakika ya 51 akimalizia pasi ya Muzamil Yassin.

Na dakika ya 74 alikuwa ni Kiungo Muzamil Yassin tena aliyeiandikia timu yake baola tatu na kuamsha shangwe za mashabiki wa Simba baada ya kuitendea haki kona ya winga Shiza Kichuya.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.