Habari za Punde

TAMASHA LA VYAKULA NA VINYWAJI KUFANYIKA LEADERS CLUB KESHO OKTOBA 8 JIJINI DAR

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya ya EM & U Investiment, Bw. Edward James akizungumza na waandishi wahabari juu ya tamasha la vinywaji na vyakula litakalofanyika viwanja Leaders Club jijini Dar es Salaam. Kushoto kwake ni Mratibu wa Tamasha hilo, Zahara Michuzi na kulia Meneja Mafunzo na Uwezeshaji, Rashid Chenja.
******************************
KAMPUNI ya EM & U Investiment imeandaa tamasha la Chakula na Vinywaji litakalofanyika (Dar es Salaam Food & Drink Festival) Jumamosi Oktoba 8, 2016 katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo Bw. Edward James amesema tamasha hilo litakuwa la aina yake kwa kushirikisha wapikaji wa vyakula vya asili ikiwa ni kufanya Watanzania kuvipenda vyakula hivyo.

James amesema kuwa watu wengi wanapenda kula vyakula vya asili lakini hawajui watavipata wapi hivyo tamasha hilo litafungua ukurasa mpya juu ya watu kuweza kupata chakula hicho na sehemu gani.

Amesema katika tamasha hilo kutakuwa na wapishi katika kila kabila kupata chakula chake cha asili katika mikoa yao hiyo itakuwa ni sehemu kuwajengea utamdauni wa kupenda chakula cha asili.

James amesema katika tamasha hilo wananchi pia watapata huduma ya kupima afyazao na magonjwa yote bure katika Tamasha hilo wasanii mbalimbali watatumbuza.
Mratibu wa Tamasha hilo Bi. Zahara Michuzi akielezea juu maandalizi ya tamasha la vinywaji na vyakula litakalofanyika Jumamosi katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.