Habari za Punde

TAYARI YAMEKWISHA ANZA YALE YALEEEEEE, HUU NDIYO UKWELI KUHUSU MISS TANZANIA 2016,DIANA

Shindano la Fainali ya Miss Tanzania 2016 limefanyika jana jijini Mwanza  ambapo mshindi ametangazwa kuwa ni Diana Lukumai, ambaye saa chache baada ya kutangazwa kwake baadhi ya watu wameonyesha kutoridhishwa na ushindi wake.

Hivi karibuni kumeibuka upotoshaji mkubwa kutoka kwa baadhi ya watu wenye nia ovu ya kutaka kuharibu taswira nzima ya Mshindi wa shindano la Miss Tanzania 2016, aliyevishwa taji hilo jana usiku ndani ya jiji la Mwanza,taarifa hizo ambazo zimekuwa zikisambazwa katika mitandao ya kijamii zikieleza upotoshwaji wa taarifa mbalimbali za mlimbwende huyo zikiwemo na elimu yake.

SEHEMU YA TAARIFA ILIYOKUWA IKIPOTOSHWA KATIKA MITANDAO MBALIMBALI YA KIJAMII HII HAPA CHINI;

MISS TANZANIA 2016
🙊🙊🙊🙊🙊🙊
JINA:Diana Edward Lukumai
UMRI:Miaka 18
ELIMU:Shahada(degree)
Hii ina maana;
Alianza Chuo akiwa na miaka 15
Alianza Form one akiwa na miaka 9
😂😂😂😂😂😂
Ingawa sio mshabiki wa haya mambo napenda nchukue hii nafasi kuwapongeza Wazazi wote kama wazazi wa Diana ambao watoto wao wameanza shule ya msingi wakiwa na miaka miwili

HII NDIO TAARIFA SAHIHI YA MSHINDI WA SHINDANO LA MISS TANZANIA 2016,DIANA EDWARD LOY.

Napenda kuujulisha Umma yafuatayo;

1. Miss Tanzania 2016/2017 aliyeshinda taji jana jijini Mwanza, anaitwa Diana Edward Loy na siyo Diana Lukumai kama inavyotajwa mitandaoni.

2. Mlimbwende huyo amemaliza kidato cha nne 2015 Shule ya Sekondari Arusha Day na si 2011 kama inavyotajwa mitandaoni kwa malengo ovu.

3. Diana hajawahi kujiunga na Elimu ya Chuo Kikuu chochote Tanzania au duniani bali anatarajia kujiunga mwaka huu katika chuo cha IFM kusomea masula ya kodi ngazi ya stashahada (cheti) ingawa kulingana na ratiba zake na majukumu yake mapya ikiwemo kushiriki Miss world mapya huenda akaahirisha mwaka wake wa masomo.

4. Tunawasihi watanzania kutumia vyema mitandao ya kijamii na si kufanya "Character assassination" lakini pia tunaheshimu haki yao ya msingi ya kuhoji masuala ya msingi kabisa kuhusu mtu ambaye ni Public figure na ataliwakilisha taifa katika anga za kimataifa.

Tumuunge mkono mlimbwende wetu ili atuletee Taji la Dunia.

Ahsanteni.

Charles William
Kaimu Ofisa Habari wake.
(wilflow101@gmail.com).
BOFYA HAPACHINI KUCHEKI VIDEO YA SHINDANO HILO JANA.

1 comment:

  1. anamiaka mingapi ndo swali la msingi, hebu tujibu

    ReplyDelete

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.