Habari za Punde

UKAWA YATANGAZA TENA KUSITISHA MAANDAMANO YA UKUTA


Mwenyekiti wa Chama cha CHADEMA Taifa Mhe. Freeman Mbowe
***********************
Na Ripota Wetu, Dar

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesitisha shughuli zote za maandamano na mikutano nchi nzima,kwa kudai kuwa ukuta ni fikra endelevu na si mpango wa siku moja.
Hayo yamesemwa leo na Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa,Mh.Freeman Mbowe wakati akizungumza na Waandishi wa Habari,Makao Makuu ya Chama hicho jijini Dar es Salaam.

Mbowe amesema kuwa wataendelea Kujipanga katika kulinda Haki yao ya kidemokrasia kama ambavyo katiba ya vyama vya siasa inavyosema,kuwa ni haki yao ya kidemokrasia.
‘’Mapambano ya kisiasa si tukio la siku moja ni tukio endelevu na kwa hiyo tarehi Mossi , Oktoba ambayo ilikuwa ni siku mbadala ya maandamano maalum,hivyo kwa niaba ya kamati kuu imeona kuna umuhimu wa kusimamisha maandamano maalumu na mikutano nchi nzima ilikupisha mbinu nyingine mbalimbali’’amesema Mbowe

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.