Habari za Punde

UP DATE YA MSIBA WA BONDIA THOMAS MASHALI, SASA KUZIKWA KESHOKUTWA JUMATANO

 Mzazi wa marehemu Thomas Mashali, Malifeza Mashali (wa pili kulia) akizungumza na aliyekuwa Promota wa mtoto wake, Kaike Siraju (kulia) wakati Promota huyo alipofika katika shughuli za msiba leo nyumbani kwa mzee huyo maeneo ya Tandale jijini Dar es Salaam. Marehemu Mashali enzi za uhai wake alishasainiana mkataba na Promota huyo wa kupanda ulingoni mwezi wa 12 kwa pambano la Ubingwa wa Dunia dhidi yake na Bondia kutoka Mawalwi Chimwemwe Chiota. Kushoto ni mdogo wa marehemu.

Katika pambano hilo ambalo lingekuwa la utangulizi lingebebwa na pambano kibwa ambapo litawakutanisha mabondia Francis Cheka na Dullah Mbabe litakalopigwa mjini Morogoro. 

Kwa mujibu wa Baba Mzazi wa marehemu, Marehemu anatarajia kuzikwa keshokutwa katika makaburi ya Kinondoni baada ya taratibu na sheria za Kipolisi kumalizika kutokana na mazingira ya kifo cha bondia huyo.
 Sehemu ya majirani ndugu na marafiki wakiwa katika msiba huo.
  Sehemu ya majirani ndugu na marafiki wakiwa katika msiba huo.
 Mzee wa marehemu akipokea simu nyingi kuhusu msiba huo leo

  Sehemu ya majirani ndugu na marafiki wakiwa katika msiba huo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.