Habari za Punde

VILABU VYA YANGA NA SIMBA VYAPIGWA 'STOP' KUENDELEA NA MCHAKATO WA MABADILIKO YA UENDESHAJI

SERIKALI kupitia Baraza la Taifa la Michezo (BMT), limepiga marufuku kuendelea kwa michakato yote ya mabadiliko ya mifumo inayofanywa na klabu za Simba na Yanga.

Agizo hilo la serikali limetolewa jana na Katibu Mkuu wa BMT, Mohamed Kiganja, alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari na kusema kuwa timu yoyote hairuhusiwi kubadili mfumo kutoka wanachama kwenda umiliki wa hisa au ukodishwaji wa hadi pale marekebisho ya katiba zao yatakapofanyiwa kazi kwa mujibu wa sheria za BMT na kanuni za msajili namba 442 kanuni ya 11 kifungu kidogo cha (1-9)yatakapofanyika.

Kiganja alisema kuwa mabadiliko hayo yanayoendelea kwenye klabu hizo tayari yameingia dosari baada ya baadhi ya Wanachama kwenda Mahakamani kupinga michakato lakini pia kupeleka malalamiko Wizara ya michezo na BMT kitu ambacho sio ishara nzuri endapo yataachwa yaendelee.
"Tumesitisha michakato yote ya kubadili umiliki kutoka kwa Wanachama kwenda kwa uwekezaji kwa timu za Simba na Yanga mpaka watakapo fanya mabadiliko kwa mujibu wa katiba za klabu zao kwa kufuata sheria zilizowekwa.

“Iwapo kama timu moja kati ya hizi zitaamua kukiuga agizo hili kwa kuendelea na mchakato huu kabla ya taratibu za kurekebisha katiba zao kisheria ni kosa na hatua stahiki zitachukuliwa dhidi ya yao,”alisema.

Alisema iwapo kama kunamdau mdau au mwanachama yoyote anayetaka kufanya uwekezaji kwenye klabu zinazomilikiwa na wanachama ni vema angeanzisha timu yake kama Saidi Bakhresa alivyoanzisha Azam FC ili kupunguza malalamiko.

Kiganja alisema kilichofanywa na klabu za Simba na Yanga ni makosa kikatiba kwani michakato hiyo ilitakiwa ianzie kwenye matawi nchi nzima ili maamuzi yawe ya wote na kama ilivyokuwa ambao inaonekana mamauzi mengi yanayotolewa yanawashirikisha wachachae.

Kiganja alisema kuwa tayari wameshapeleka barua Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) juu ya kuzuia jambo hilo ili waweze kuwapa taarifa wanachama wao na wanahakika hakuna atakayefanya jambo kinyume na maamuzi ya serikali inayoongozwa kwa kutumia katiba.

Kuali hiyo ya serikali imekuja baada ya miezi michache kupita Klabu ya Simba ku taka kuingia katika mfumo wa hisa kwa kumkabidhi timu mfanyabiashara mkubwa Afrika , Mohamed Dewij(MO) ambaye anataka asilimi 51 huku wanachama wakibaki na 49.

Wakati hali ikiwa hivyo kwa Wanamsimbazi, Jangwani nako kupitia mkutano wao mkuu uliofanyika Agosti 6 mwaka huu, walilidhia ombi la mwenyekiti wao kuikokodisha Yanga kwa miaka 10 kwa kuchukua timu na nembo huku kila mwaka akiwapa asiliami 25 ya faida na yeye kubaki na 75.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.