Habari za Punde

WADAU WA LUGHA WAPONGEZWA KWA KUKUZA, KUENEZA NA KUIMARISHA LUGHA YA KISWAHILI

 Naibu Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James Wambura (kushoto) akizungumza na Wadau wa Lugha ya Kiswahili (hawapo pichani) wakati wa kikao na wadau hao kujadili changamoto zinazokabili Tasnia ya Lugha nchini na kuzipatia ufumbuzi leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Lugha Hajjat Shani Kitogo
 Mkurugenzi Msaidizi Lugha Hajjat Shani Kitogo akifafanua jambo wakati wa kikao na wadau wa Lugha ya Kiswahili kujadili changamoto zinazokabili Tasnia ya Lugha nchini na kuzipatia ufumbuzi leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Naibu Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James Wambura
Mwandishi wa Vitabu vya Riwaya Bw. Adam Shafi (aliyesimama) akichangia mada wakati wa kikao na wadau wa Lugha ya Kiswahili kujadili changamoto zinazokabili Tasnia ya Lugha nchini na kuzipatia ufumbuzi leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mmiliki wa kampuni ya machapisho ya Mkuki na Nyota Bw. Walter Bgoya
 Wadau mbalimbali wa Lugha ya Kiswahili wakijadiliana wakati wa kikao na Naibu Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James Wambura (kushoto) kujadili changamoto zinazokabili Tasnia ya Lugha nchini na kuzipatia ufumbuzi leo Jijini Dar es Salaam.
Mshairi mama Mipango akiimba shairi la kuipongeza Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kusimamia vizuri Lugha ya Kiswahili katika kuikuza na kuieneza wakati wa kikao na wadau wa Lugha ya Kiswahili kujadili changamoto zinazokabili Tasnia ya Lugha nchini na kuzipatia ufumbuzi leo Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James Wambura (katikati waliokaa) katika picha ya pamoja na Wadau wa Lugha ya Kiswahili wakati wa kikao na wadau hao kujadili changamoto zinazokabili Tasnia ya Lugha nchini na kuzipatia ufumbuzi leo Jijini Dar es Salaam. Kulia waliokaa ni Mkurugenzi Msaidizi Lugha Hajjat Shani Kitogo na kushoto waliokaa ni Mjumbe kutoka Idara ya Lugha na Fasihi Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) Bibi. Gertrude Joseph. Picha na: Genofeva Matemu - WHUSM
*********************************************************
Na: Genofeva Matemu – WHUSM
Wadau wa Lugha ya Kiswahili nchini wamepongezwa kwa kazi kubwa na nzuri wanazozifanya za kukuza, kueneza, kuimarisha na kuendeleza lugha ya Kiswahili kwani wamekifanya Kiswahili kuwa lugha yenye mawasiliano mapana katika nchi za Afrika Mashariki, Afrika na Dunia nzima.

Hayo yamesema na Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James Wambura wakati wa kikao na wadau hao kujadili changamoto zinazokabili Tasnia ya Lugha nchini na kuzipatia ufumbuzi leo Jijini Dar es Salaa.

“Vyama mbalimbali vya kukuza na kueneza Lugha ya Kiswahili nchini kwa kushirikiana na wadau mbalimbali mmekua kichocheo kikubwa cha kuendeleza lugha ya Kiswahili na kuisambaza kwa kasi hata kuweza kuvuka mipaka ya Tanzania” amesema Mhe. Anastazia.

Mhe. Anastazia amewataka wadau wa Lugha ya Kiswahili kushiriki vema katika mijadala itakayokua inaandaliwa ya lugha hiyo ili waweze kutoa maoni na mapendelkezo fahafu yenye lengo la kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali, Taasisi, Asasi na vyama mbalimbali vya wadau wa lugha ya Kiswahili nchini.

Kwa upande wake Mkuregenzi kutoka Chama cha Kiswahili na Sanaa (KINASA) Bw. Mutalemwa Jason ameiomba serikali kuhakikisha kuwa utamaduni wa Vilabu vya Kiswahili kwa shule za msingi na sekondari unarejeshwa ili kutoa fursa nzuri kwa wanafunzi kukutana na kujadili misamihati mbalimbali ya Kiswahili.  

Naye Naibu Katibu Mkuu kutoka Umoja wa Washairi Tanzania (UWASHATA) ameviomba vyombo vya habari nchini kusaidia kurusha mashairi yanaimbwa na wadau wa lugha ya Kiswahili kwani kwa kufanya hivyo watawezesha misamihati ya lugha ya Kiswahili kuenea kwa kasi ndani na nje ya nchi.

Tangu tulipopata uhuru mwaka 1961 masuala  yahusuyo Lugha katika nchi yetu yamezingatiwa kama kipengele muhimu katika Sera ya Utamaduni ya mwaka 1997, Serikali ya awamu ya tano imezingatia umuhimu mkubwa wa kuwa na Sera ya Taifa ya Lugha ambayo ni muongozo dhabiti inayosimamia masuala yote yanayohusu Lugha nchini ambapo kwa sasa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo inaendelea na mchakato wa uandaaji wa rasimu ya Sera ya Taifa ya Lugha katika hatua ya ukusanyaji wa maoni ya wadau wa Lugha hiyo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.