Habari za Punde

WAKAZI WA BUNJU BEACH WAHAKIKISHIWA ULINZI USALAMA

RPC wa Kinondoni Suzan Kaganda akizungumza na wanajumuiya ya Bunju Beach Community Support wakati wa hafla ya kujumuika pamoja kwa wanajumuiya hao hivi karibuni Jijini Dar es Salaam.Kutoka kulia ni Diwani wa Kata ya Bunju Mhe. Phocas Nato, OCD Kawe, John Malulu na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Bw. Kheri Nassor Missinga. 
Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya wakazi wa Bunju Beach,Bunju Beach Community Support Bi. Vanessa Milinga akisoma risala ya Jumuiya hiyo wakati wa hafla ya kujumuika pamoja kwa wanajumuiya hivi karibuni Jijini Dar es Salaam.
RPC wa Kinondoni Suzan Kaganda akipeana mkono na Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya wakazi wa Bunju Beach (Bunju Beach Community Support) Bi. Vanessa Milinga mara baada ya kumkabidhi risala wakati wa hafla ya kujumuika pamoja kwa wanajumuiya hao hivi karibuni Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Diwani wa Kata ya Bunju Mhe. Phocas Nato na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Bw. Kheri Nassor Missinga.
RPC wa Kinondoni Suzan Kaganda wakigonga cheers wakati wa hafla ya kujumuika pamoja kwa wanajumuiya hao hivi karibuni Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Diwani wa Kata ya Bunju Mhe. Phocas Nato na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Bw. Kheri Nassor Missinga.
Muasisi wa Jumuiya ya Bunju Community Support Profesa. Joas Rugemalila (kushoto) akigonga cheers na RPC wa Kinondoni Suzan Kaganda wakati wa hafla ya kujumuika pamoja kwa wanajumuiya hao hivi karibuni Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Diwani wa Kata ya Bunju Mhe. Phocas Nato na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Bw. Kheri Nassor Missinga. Na Mpiga Picha Wetu.
**************************************************
Na: Mwandishi Wetu.
SUALA la wizi na ujambazi kwa wakazi wa Bunju Beach kubakia kuwa historia baada ya Jeshi la Polisi wilaya ya Kinondoni kuahidi kujenga kituo cha Polisi kitakachokuwa na uwezo wa kuchukua Askari zaidi ya 40. 

Hayo yamebainishwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, ACP Suzan Kaganda alipokuwa mgeni rasmi katika hafla ya kuzindua umoja wa Wakazi wa Bunju “Bunju Beach Community Support” 

RPC Kaganda amesema kuwa wezi na majambazi wamekula kwao na kuongeza kuwa suala la ulinzi na usalama ni la kila raia kwa mujibu wa sheria. 

Awali akisoma risala ya Jumuiya hiyo Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya kusaidiana ya Wakazi wa Bunju (Bunju Beach Community Support), Vanessa Milinga alisema kuwa Jumuiya hiyo ilianzishwa mwaka 2005 ikiwa na lengo la kuimarisha ulinzi na usalama wa mali na familia za wakazi wa Bunju Beach.

Vanessa amesema kuwa mwaka 2011 walipata usajili ambapo pia wanachama wameongezeka na kupelekea kubadili kuongezeka kwa malengo ambayo ni pamoja na kuanzishwa kwa SACCOSS.

Akizungumzia historia ya Bunju Beach Community Support, Mmoja wa waanzilishi wa Jumuiya hiyo Profesa. Joas Rugemalila amesema kuwa umoja huo umeanzishwa kwa lengo la kuimarisha ulinzi shirikishi, usalama, amani na maendeleo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.