Habari za Punde

WANAFUNZI WA SHULE ZA SEKONDARI WATAKIWA KUWA MABALOZI WA ELIMU YA MPIGA KURA.

 Mwanasheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),Bi. Fausta Mahenge akitoa elimu ya mpiga kura kuhusu masuala mbalimbali ya kisheria yanayosimamia chaguzi za Tanzania kwa wanafunzi 743 wa  Shule ya Sekondari Kidinda wilayani Bariadi mkoani Simiyu.
 Afisa Uchaguzi wa NEC Bw. Stephen Elisante akiwaonyesha wanafunzi wa shule ya Sekondari Kidinda fomu maalumu zinazotumika kujaza matokeo ya uchaguzi katika vituo vya kupigia kura wakati akitoa elimu ya Mpiga Kurra kwa wanafunzi wa shule hiyo, Bariadi mkoani Simiyu.
 Afisa Uchaguzi wa NEC Bw. Stephen Elisante akisisitiza jambo kwa wanafunzi wa shule ya Sekondari Kidinda wakati akitoa elimu ya Mpiga Kurra kwa wanafunzi wa shule hiyo, Bariadi mkoani Simiyu.
 Makamu Mkuu wa Shule ya Sekondari Kidinda Mwalimu Paul Susu akizungumza na wanafunzi wa shule hiyo mara baada ya kuwakaribisha Maofisa wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi waliofika shuleni hapo kutoa Elimu ya Mpiga Kura kwa wanafunzi wapatao 743 wa shule hiyo.
 Mwanafunzi wa Kidato cha tatu wa shule ya Sekondari Kidinda, Filipo Madeni akiwauliza swali Maofisa wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuhusu mfumo unaotumika kuwapata wagombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mwanasheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),Bi. Fausta Mahenge akiwaonesha mfano wa karatasi inayotumika kupigia kura yenye majina ya wagombea wa vyama mbalimbali wakati akitoa elimu ya Mpiga Kura katika Shule ya Sekondari Kidinda wilayani Bariadi mkoani Simiyu. 

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.