Habari za Punde

WANAFUNZI WIZARA YA ELIMU WALALAMA KUPUNGUZIWA MKOPO

Naibu wa Waziri wa Mikopo wa Serikali ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam(Daruso), Kasunzu Apolinary akizungumza na waandishi wa habari juu ya kufika katika Wizara ya Elimu kudai kupunguzwa mkwa mkopo katika bodi ya mikopo leo jijini Dar es Salaam.
***********************************************8
Na Anthon John, Dar
WANAFUNZI wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam wameandamana leo katika Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia kudai mkopo kuongezwa kutokana na gharama za maisha kupanda.

Wakizungumza katika Jengo la Wizara hiyo, wamesema kuwa kuwa kiwango cha mkopo ni kidogo hakiwakimu katika kuendesha maisha ya chuo.

Naibu wa Waziri wa Mikopo wa Serikali ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam(Daruso), Kasunzu Apolinary amesema maisha ni magumu kutokana na bodi ya mikopo kupunguza mkopo na kufikia sh. 510000 na hadi kufikia sh.19266 kwa miezi miwili.

Amesema kuwa wanafunzi kuwa sasa wanatakiwa kutumia sh.320 kwa siku kwa muda wa miezi miwili kwa fedha ya mkopo huo.

Apolinary ameasema maisha yamekuwa ni magumu na kufanya baadhi ya wanafunzi wengine kushindwa kulipa pango ya nyumba na kufanya kuanza kulanda landa katika viwanja vya chuo.

Baada ya wanafunzi hao kufika katika jengo la Wizara hiyo nia ya kukutana na Waziri mwenye dhamana ya elimu ziligonga mwamba na kuambiwa warudi wanalifanyia kazi suala hilo.
Sehemu ya wanafunzi wakiwa katika viyunga vya wizara ya elimu kudai kupunguzwa kwa mikopo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.