Habari za Punde

WANAHABARI WAPIGWA MSASA KUHUSU KINGATIBA YA MABUSHA, MATENDE, USUBI, KICHOCHO, TRAKOMA
Ofisa Mradi wa Mpango wa Magonjwa Yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele, Oscar Kaitaba akielezea umuhimu wa vyombo vya habari kuelimisha umma kujenga tabia ya kutumia Kingatiba ya magonjwa ya kichocho, Minyoo ya Tumbo, Usubi Matende na Mabusha wakati wa Warsha iliyoshirikisha wanahabari, Dar es Salaam leo. Kampeni ya kuwapatia wananchi Tibakinga kwa wakazi takribani mil. 4 wa Jiji la Dar es Salaam itaanza Oktoba 25 waka huu. 

Meneja Mradi wa Mpango wa Magonjwa Yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele, Upendo Mwingira akifafanua jambo wakati wa warsha hiyo. KWA PICHA ZAIDI BOFYA READ MORE

Wanahabari wakiwa katika warsha hiyo
Mtangazaji wa BBC, Halima Kassim akitafakari jambo kuhusu semina hiyo ya wanahabari kupata uelewa kuhusu magonjwa hayo na jinsi ya kuwaelimisha wananchi kutumia Kingatiba kwa kumeza dawa mara noja kila mwaka ili kuboresha afya.


Mtaalamu Kaitaba akionesha baadhi ya dawa za Kingatiba ya magonjwa hayo.


Ofisa Habari wa Mradi huo, Said Makora akiwataka wanahabari kuwaelimiasha wananchi juu ya magonjwa hayo na jinsi ya kupata Kingatiba kwa kuandika makala, habari, majarida na kutumia mitandao ya kijamii kwa nia ya kuyatokomeza magonjwa hayo kufikia mwaka 2020.

Kaitaba akionesha vifaa vinavyotumika kuwapima watu ili wapewe dawa kulingana na kimo chake.

Mwandishi wa Habari wa Nipashe, Yasmin Protas, akichangia mada wakati wa semina hiyo.

Wana habari wakipatiwa dawa za Kingatiba za magonjwa hayo


Mtangazaji wa E FM Radio akipimwa urefu ndipo apatiwe dawa. PICHA NA RICHARD MWAIKENDA

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.