Habari za Punde

WAZIRI MWIGULU AKUTANA NA WAKUU WA TAASISI NA IDARA WA WIZARA YAKE.

Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, akizungumza na wakuu wa Taasisi na Idara za wizara (hawapo pichani), wakati wa kikao cha  kujadili masuala mbalimbali ya mipango na maendeleo ya wizara. Kulia ni Naibu Waziri  Mhandisi Hamad Masauni. Kikao hicho kimefanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa wizara, jijini Dar es Salaam.
 Wakuu wa Taasisi na Idara za Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi; Jeshi la Polisi, Jeshi la Magereza, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Idara ya Uhamiaji, Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Idara ya Wakimbizi pamoja na wakuu wa vitengo wizarani hapo wakimsikiliza Waziri wa wizara hiyo, Mwigulu Nchemba, wakati kikao cha kujadili masuala mbalimbali ya mipango na maendeleo ya wizara. Kikao hicho kimefanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa wizara, jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu, akizungumza wakati  wa kikao cha  kujadili masuala mbalimbali ya mipango na maendeleo ya  Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na Idara zake. Kikao hicho kiliongozwa na Waziri wa wizara hiyo, Mwigulu Nchemba (hayupo pichani). Kushoto ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Minja. Kikao hicho kimefanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa wizara, jijini Dar es Salaam .Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.