Habari za Punde

YANGA YATOA DOZI YA 3-1 KWA MTIBWA SUGAR, CHIRWA 'AANZA KAMA POGBA', SIMBA YAWAADHIBU MBEYA CITY NYUMBANI 2-0

Mshambuliaji wa Yanga,Obrey Chirwa leo amenza kuwashawishi mashabiki wa timu yake baada ya kuifungia timu yake baola kuongoza katika dakika ya 44 kipindi cha kwanza dhidi ya Mtibwa Sugar mchezo uliopigwa jioni leo kweny Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. 

Katika mchezo huo Yanga wameibuka na ushindi wa mabao 3-1 huku baola kwanza likifungwa na Obrey Chirwa, la pili Simon Msuva katika dakika ya 68 na baola tatu likifungwa na Donald Ngoma katika dakika ya 80 akitokea benchi kuchukua nafasi ya mfungaji wa baola kwanza Obrey Chirwa.

Bao la kufutia machozi la Mtibwa Sugar lilifungwa na Haruna Chanongo katika dakika ya 63.

Yanga walifanya mabadiliko kipindi cha pili kwa kumtoa Deus Kaseke na kuingia Geofrey Mwashiuya, na kutoa pasi ya bao la tatu.
Yanga sasa inafikisha pointi 14 baada ya kucheza mechi saba, huku ikizidiwa pointi sita na mahasimu wao wa jadi, Simba SC walio kileleni na pointi zao 20 baada ya mchezo wa leo walioshinda 2-0 dhidi ya Mbeya City.

MATOKEO MENGINE YA MECHI ZA LEO:
Yanga 3 - Mtibwa Sugar 1
Mbeya City 0 - Simba 2
Stand United 1 - Azam Fc 0
Mwadui Fc 2 - African Lyon 0
Mbao Fc 3 - Toto African 1
Maji Maji 0 - Kagera 1
JKT Ruvu 0 - Tanzania Prisons 0

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.