Habari za Punde

ZIARA YA JAJI MKUU WA AUSTRALIA YA KUSINI NCHINI AKUTANA NA JAJI MKUU OTHMAN CHANDE.

 Jaji Mkuu wa Australia  ya Kusini, Mhe. Christopher Kourakis (kushoto), akizungumza jambo na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman (kulia) katika ofisi ya  Jaji Mkuu wa Tanzania, iliyopo kwenye jengo la Mahakama ya Rufani Tanzania, jijini Dar es Salaam. Mhe. Jaji Kourakis yupo nchini kwa ziara ya siku tatu yenye lengo la kujenga ushirikiano katika utendaji kazi wa Mahakama baina  ya nchi hizo mbili. Kushoto ni Bi. Emma Gorman, Katibu wa Jaji Mkuu wa Australia Kusini tarehe. 5.10.2016.
Jaji Mkuu wa Australia ya Kusini, Mhe.Christopher Kourakis (kushoto)    akisoma kitabu kinachohusu Chama cha Majaji Wanawake   Tanzania wakati alipotembelea ofisini kwa Mwenyeji wake Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman tarehe. 5.10.2016.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.