Habari za Punde

BAADA YA KUWAPIGA YANGA, KOCHA WA MBEYA CITY KINNAH PHIRI AWASHUKURU MASHABIKI WAKE

Siku moja baada ya kuiduwaza Yanga kwa kipigo cha bao 2-1,kocha mkuu wa Mbeya City fc Kinnah Phiri amejitokeza na kuwapongeza mashabiki wa timu hiyo kwa namna walivyojitokeza kwa wingi na kuishangilia timu yao muda wote wa mchezo jambo lililoanikiza ushindi huo.

Akizungumza na mtandao huu leo asubuhi, Kocha Phiri alisema kuwa nguvu kubwa ya ushangiliaji iliyokuwa inatoka upande wa jukwaa la mashabiki wa City iliwafanya wachezaji kutambua kuwa wanalo jukumu kubwa la kucheza kwa nguvu na umakini mkubwa kuhakikisha wanapata matokeo ambayo yangekuwa faraja pekee kwa mashabiki wao waliojitopkeza uwanjani kwa wingi.

“Hakika ilikuwa siku nzuri, mashabiki walijitokeza kwa wingi, nguvu yao ya ushangiliaji ilistua mioyo ya wachezaji wangu wakatambua kuwa wanadeni kubwa la kusherehesha furaha kwa mashabiki wao kwa kufanya jambo moja tu la kucheza kwa nguvu na umakini kuhakikisha wanashinda na kupata pointi tatu kutoka moyoni ninawashukuru sana walifanya kazi kubwa” alisema.

Kuhusu hali ya kikosi na mpango wa kushinda mchezo huo kiufundi, Kocha Phiri alisema kuwa, awali aligundua nguvu kubwa ya Yanga inatoka pembeni ya uwanja huku akianikizwa na viungo wa katikati hivyo alilazimi kubadili mfumo na kikosi kuhakikisha timu hiyo ya Dar es Salaam haipati mwanya wa kupita au kutengeneza nafasi ya kufunga bao.

“Yes!nilifanya maamuzi mengi tofauti hii ni baada ya kuifuatilia Yanga kwenye michezo kadhaa,nilibadilisha kikosi nikabadilisha mfumo,Yanga ni timu nzuri huwezi kuiweka kwenye kundi la timu ndogo lakini ubora wetu kwenye mchezo wa jana uliwanyima nafasi ya kucheza mchezo wao waliouzoea na kushindwa kuleta hatari langoni kwetu,vijana wangu walicheza kwa namna nilivyowaelekeza ndiyo sababu kila mmoja aliona tumecheza vizuri ” alisema.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.