Habari za Punde

BOKO BEACH VETERANS YAIRARUA BUNJU VETERANS MABAO 6-1 MCHEZO WA KIRAFIKITimu ya Boko Veterans ikiwa katika picha ya pamoja kabla ya mchezo wa kirafiki dhidi yao na Bunju Veterans jana. Katika mchezo huo Boko Veterans ilishinda mabao 6-1.

Timu ya Boko Beach Veterans (BBV) imeeendeleza ubabe wake baada ya kuichapa Timu ya Veterans ya Bunju kwa jumla ya magoli 6-1 na kuendeleza kuweka rekodi ya kutofungwa katika michezo mitano. BBV imeshazitadika Timu za Tabora Veterans, BOT Veterans, Mbezi Veterans na Veteran ya Jeshi Lugalo, na kufanya kuwa tishio kwa timu zingine ambazo zinatafakari ni namna gani wataikabili timu hiyo vinara wa Maveterans.

Dalili za mvua hiyo zilianza mapema katika kipindi cha kwanza baada ya kazi nzuri ya kiungo Lazaro Ngimba kuihadaa beki ya Bunju na kutoa pasi nzuri kwa Bruce Mwile ambaye bila ajizi alitupia kambani, baada ya goli hilo BBV waliendelea kuishambulia ngome ya BUNJU kama nyuki na kufanikiwa kufunga magoli mengine kupitia kwa Lazaro Ngimba, Holombe Jr, Hebron Malakasuka na Bruce Mwile aliefunga hat trick. 

Katika mchezo huo uliotawaliwa na BBV ambayo ilionyesha uwezo mkubwa iliwakilishwa na golikipa Dihile, Mabeki Mango, Msaki, Robert, Kairuki, viungo Lazaro, Rodric Mwambene, Deo Ringia, Horombe Jr, Mawinga Ole aka Aguerro, Richard, Chief Ndabile na striker Bruce, Edwin aka Mavugo na Wengine waliotokea Katika bench.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.