Habari za Punde

BONDIA THOMAS MASHALI KUZIKWA KESHO MAKABURI YA KINONDONI

 Mmoja kati ya Wadau wa mchezo wa ngumi nchini, Anthony Lutta, akisoma habari ya marehemu Thomas Mashali katika gazeti la michezo la Bingwa, wakati akiwa katika shughuli ya msiba huo nyumbani kwa mzazi wa mareheu maeneo ya Tandale jijini Dar es Salaam, mchana huu.

Marehemu Mashali anatarajia kuzikwa kesho katika Makaburi ya Kinondoni, huku wadau,ndugu na Jamaa wa marehemu wakiendelea na vikao vya kuweza kufanikisha shughuli hiyo ya maziko ambapo inatazamiwa shughuli za kuaga mwili wa marehemu zikafanyika Viwanja vya Leaders Club Kinondoni ikiwezekana. 
 Bondia Joseph Kaseba akizungumza na baadhi ya Mabondia wenzake nyumbani kwa marehemu Mashali wakipanga mikakati ya kikao cha pamoja watakachofanya leo majira ya saa tisa jioni kuhusu shughuli za maziko.
Sehemu ya wadau wa mchezowa ngumi na ndugu na majirani wakiwa katika msiba huo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.