Habari za Punde

DC KASULU AKERWA NA WAFUGAJI WANAOHARIBU MSITU WA KAGERANKANDA

Na FK Blog- Kigoma
MKUU wa Wilaya ya Kasulu Kanali Martin Mkisi ameeleza kukerwa na tabia ya wakulima na wafugaji wanaovamia hifadhi ya Msitu wa Kagerankanda na kufanya shughuli za ufugaji na kilimo katika msitu huo wenye sifa pekee ya Uoto wa Asili Mkoani Kigoma.

Kauli hiyo aliitoa mwishoni mwa wiki katika kikao cha Baraza la madiwani kilichokuwa kikiwasilisha taarifa mbalimbali za utendaji kazi wa kamati husika katika kipindi cha Julai-Septemba 2016, ambapo mkuu huyo wa Wilaya alitumia nafasi hiyo kuwaasa madiwani wahamasishe wananchi wapishe hifadhi hiyo kabla ya kutumika nguvu ya ziada.

Kanali Mkisi alisema changamoto ya uvamizi katika msitu huo ni ya muda mrefu na kueleza kusikitiswa na vitendo hivyo kutokana na kuwa vitendo hivyo ni janga kwa kizazi cha kijacho, kutokana na makundi ya wakulima na wafugaji kuendelea kujazana katika msituni huo kwa shughuli za kilimo na ufugaji wakati kuna maeneo makubwa yapo wazi na yana rutuba kwa uzalishaji wa bidhaa zao. 

“mimi ni kanali siendeshi wilaya kiraia ,nataka sheria,kanuni na taratibu zitumike katika kurasimisha makazi si kuvamia misitu ya asili yenye hadhi ya uoto wa asili na mimi niseme ukweli, nashangzwa na baadhi ya viongozi wanalifumbia macho wakati rasilimali inatumiwa hovyo kwa maslahi yenu binafsi” alisema
Aidha Mkisi alisema, hatojali zengwe kwa kuwa amechaguliwa na serikali hivyo nitasimamia sheria, kanuni na taratibu husika, na kusema kuwa aliondolewa katika nafasi yake huku akiwa anasimamia sheria na kanuni hatosita kuendelea na shughuli nyingine.

Akizungumzia kero ya uvamizi wa hifadhi hiyo Diwani wa kata ya Kagerankanda Ezekieli Mshingo, alikiri wananchi kutumia msitu huo kwa zaidi ya miaka 12 kama kichaka cha wahamiaji haramu,ufichwaji wa silaha haramu za moto pamoja na makundi ya wafugaji na wakulima kuongezeka kila kukicha.

Mshingo alisema uvamizi unatokana na usimamizi mbovu kuanzia ngazi ya juu hadi ya chini na kitendo cha kuwaondoa makundi hayo katika msitu wa kagerankanda ni changamoto kwa kuwa, wavamizi wengi wanasaidiwa na watu wakubwa hali inayochangia mauwaji kila mwaka na kutolea mfano wa Novemba 3, 2016 kuna mfugaji mmoja Majigwa Magesa ameuwawa na mwishoni na kwamba hakuna hatua zilizochukuliwa dhidi ya waharifu.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu vijijini Yohana Mshita alisema taifa lilipofikia linahitaji kiongozi muwazi, mkweli mwenye moyo wa dhati katika kuondoa kero za wananchi kwa uadilifu huku akifuata sheria zilizopo lengo lkiwa ni kutimiza malengo yake na kusema kuwa katika utendaji huo baadhi ya watendaji wa halmashauri za wilaya wamekua na taba ya majungu ya kukwamisha utekelezaji wa shughuli mbalimbali hivyo kumuomba mkuu huyo kutosikiliza maneno yao.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.