Habari za Punde

DK. SHEIN ASAINI SHERIA YA MUSWADA WA MAFUTA ZANZIBARRais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akitia saini muswada wa sheria ya Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi asilia ya mwaka 2016, katika hafla iliyofanyika leo ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,ambapo Viongozi mbali mbali wa Serikali na vyama vya Siasa walihudhuria hafkla hiyo.
***************************************************
Na Dk. Juma Mohammed,  MAELEZO Zanzibar


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohammed Shein amesaini Mswada wa sheria ya utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia na kusisitiza kwamba Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haikuvunjwa.
Akizungumza Ikulu Mjini Zanzibar jana wakati akitia saini Mswada wa sheria ya utafutaji, uchimbaji wa mafuta na gesi asilia wa mwaka 2016, Rais Dk. Shein alisema kwamba taratibu zote zimefuatwa wakati wa mchakato wa kutunga kwa sheria hiyo na kuwaomba wananchi kuwapuuza wanaoeneza uzushi.
Rais Dk. Shein alisema haja ya kuwepo kwa sheria hiyo inatokana na masharti ya kifungu cha nne Sheria ya Mafuta na Gesi Asilia 2015 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo inataja kwamba shughuli za uendeshaji wa Mafuta na Gesi Asilia utafanywa Zanzibar kwa kusimamia na kuendeshwa na taasisi kwa mujibu wa Sheria za Zanzibar.
“Kumekuwa na maneno mengi kwamba nisisaini sheria hii, Hakuna katiba wala sheria iliyovunjwa na tunawaomba wananchi kuendelea kuwa watulivu, kuheshimu sheria na kudumisha amani na mshikamano” Alisisitiza Rais Dk. Shein.
Rais Dk. Shein amewataka wananchi wasikubali kuyumbishwa na wala wasibabaishwe na watu wasioitakia mema Zanzibar. Alisema kwamba sheria hiyo sasa itafungua milango kwa Makampuni mbalimbali kujitokeza kuanza kazi ya utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asili Visiwani Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akionesha hati muswada wa sheria ya Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi asilia ya mwaka 2016,baada ya kusaini hati hiyo katika hafla iliyofanyika leo ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,ambapo Viongozi mbali mbali wa Serikali na vyama vya Siasa walihudhuria hafkla hiyo.
Viongozi Wakuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama Zanzibar wakiwa katika hafla ya utiaji saini muswada wa sheria ya Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi asilia ya mwaka 2016,uliotiwa leo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja
Baadhi ya Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi na Viongozi mbali mbali wakiwa katika hafla ya utiaji saini muswada wa sheria ya Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi asilia ya mwaka 2016,uliotiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo
Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe,Zubeir Ali Maulid (kulia) na Waziri wa Nishati na Madini Mhe,Profesa Sospiter Muhongo,wakiwa katika hafla ya Utiaji wa saini muswada wa sheria ya Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi asilia ya mwaka 2016,uliotiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.