Habari za Punde

DKT MGWATU APONGEZA UTENDAJI KAZI WA TEMESA LINDI.

 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme – TEMESA Dkt Mussa Mgwatu (kulia) akiongea na Meneja wa TEMESA Lindi Mhandisi Grayson Maleko (kushoto) alipotembelea kituoni hapo.
 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme – TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu (kushoto w) akiongea na watumishi wa Karakana ya TEMESA Lindi, alipotembelea kituoni hapo mapema.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme – TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu akiangalia eneo litakalojengwa gati  kwa ajili ya Kivuko cha Lindi Kitundamkoani Lindi. Picha na Theresia Mwami TEMESA Lindi
********************************************************
Na Theresia Mwami TEMESA Lindi
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania – TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu amepongeza utaratibu unaotumika katika kituo cha TEMESA Lindi na karakana zake kwa kuratibu vizuri kazi za kila siku. 
“Nawapongeza sana kwa utendaji wenu wa kazi kwa kuweka utaratibu wa kufuatilia kila kazi inayofanywa na wafanyakazi wa kituo” alisema  Dkt. Mgwatu.
Dkt Mgwatu amemuagiza  Meneja wa TEMESA Mkoa wa Lindi Mhandisi Greyson Maleko kuhakikisha kuwa magari yote ya Serikali mkoani Lindi yanafanyiwa matengenezo katika karakana ya TEMESA iliyopo mkoani humo.
Dkt. Mgwatu amemtaka Meneja huyo kuhakikisha anakusanya madeni yote wanayodai kwenye Taasisi, Halmashauri na Idara mbalimbali za Serikali kutokana na matengenezo ya magari na mitambo, sambamba na kulipa madeni yote wanayodaiwa na wazabuni kwa kipindi cha Julai-Septemba, 2016.
Kwa upande wake Meneja wa TEMESA Lindi alisema kuwa changamoto kubwa inayokabili kituo hicho ni uwepo wa madeni makubwa wanayodai kwenye Taasisi na Halmashauri mbali mbali za serikali zilizopo Mkoani Lindi kutokana na matengenezo ya magari na mitambo lakini wanajitaidi kuendelea kufanya kazi kwa ustadi na kujituma.
Katika hatua nyingine Dkt. Mgwatu alitembelea eneo litakalojengwa gati kwa ajili ya kivuko kutoka Lindi hadi Kitunda.
Dkt. Mgwatu yupo katika ziara ya kikazi kutembelea mikoa ya Lindi na Mtwara ili kujionea hali ya Vituo katika mikoa hiyo pamoja na utendaji kazi wake.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.