Habari za Punde

DTB KUSOMESHA SEKONDARI WATOTO WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU

Bi. Sheena Sinare, (katikati) Afisa wa Diamond Trust Bank (DTB), akikabidhi malipo kwa ajili ya ada ya wanafunzi 5 kwa mkurugenzi wa shule ya Sekondari ya Sullivan Provost iliyopo Kibaha Mkoa wa Pwani. Bi. Rachel Mwalukasa. 

Wanafunzi hao kutoka katika Makao ya Watoto yatima Kurasini ni– Fadhili Dotto (14), Bakari Majuto (14) , Justin Msafiri (15), Baltadhar Steward (14) na Omary Ramadan (16). Kushoto ni Bi. Beatrice Mgumiro, Msimamizi wa Makao ya watoto yatima Kurasini na Kulia ni Mwalimu Mkuu wa shule ya Sullivan Provost, Nd. Alex Nicholaus Sibuti. Wanafunzi hao wanajiunga na shule ya bweni ya Sullivan Provost katika kidato cha kwanza mwakani, na tayari wameanza masomo ya awali (Pre-Form one).
Ilikuwa ni Furaha tele wakati Diamond Trust Bank (DTB), walipotoa udhamini wa kuwasomesha watoto 5 kutoka Makao ya Watoto yatima Kurasini. Wanafunzi hawa watakaojiunga na shule ya Sekondari ya Sullivan Provost iliyopo Kibaha Mkoa wa Pwani mwakani, tayari wameanza masomo ya awali (pre form one). 

Benki ya DTB Tanzania kwa kupitia kitengo cha huduma za kijamii, imegharamia mahitaji mengine yote pamoja na ada ya hawa vijana ili waweze kusoma vizuri. katika mstari wa nyuma ni Fadhili Dotto (14), Bakari Majuto (14) , Justin Msafiri (15), Baltadhar Steward (14) na Omary Ramadan (16). Walioketi mstari wa mbele kushoto ni Bi. Sheena Sinare, Afisa kutoka DTB Tanzania, Bi. Beatrice Mgumiro, Msimamizi wa Makao ya watoto yatima Kurasini, Bi. Rachel Mwalukasa, mkurugenzi wa shule ya Sekondari ya Sullivan Provost, Nd. Alex Nicholaus Sibuti, Mwalimu Mkuu na Bi. Monica Nangale, Afisa toka benki ya DTB Tanzania.
Afisa wa Benki ya Diamond Trust Bank (DTB) , Bi. Sheena Sinare (katikati) , akiwa pamoja na watoto kutoka Makao ya Watoto yatima Kurasini. Kulia ni Bi. Rachel Mwalukasa, Mkurugenzi wa shule ya Sekondari ya bweni - Sullivan Provost iliyopo Kibaha Mkoa wa Pwani na kushoto ni Bi. Beatrice Mgumiro, Msimamizi wa Makao ya watoto yatima Kurasini. DTB imetoa ada ya mwaka mmoja kwa wanafunzi 5 kutoka katika hicho kituo ambao ni Fadhili Dotto (14), Bakari Majuto (14) , Justin Msafiri (15), Baltadhar Steward (14) na Omary Ramadan (16) ambao wote wapo katika picha. 

Wanafunzi hao wanajiunga na shule ya bweni ya Sullivan Provost katika kidato cha kwanza mwakani, na tayari wameanza masomo ya awali (Pre-Form one).

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.