Habari za Punde

KANDANDA DAY YAKABIDHI MADAWATI 20 KWA SHULE YA MSINGI UBUNGO PLAZA

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Anthony Peter Mavunde akiwa pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam, wakati wa hafla ya kukabidhi madawati 20 yaliyotolewa na Mtandao wa Wapenda soka wa Kandanda kwa shule hiyo. Hafla hiyo imefanyika Novemba 26, 2016 jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Anthony Peter Mavunde akifurahi jambo na wanfunzi hao mara baada ya kukabidhi madawati.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Anthony Peter Mavunde akizungumza kabla ya kukabidhi madawati 20 yaliyotolewa na Vijana wa Mtandao wa Kandanda.
Mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Ubungo Plaza,Renatus Pathi akizungumza wakati wa hafla ya kupokea madawati iliyofanyika shuleni hapo
Mratibu kutoka Kundi la Kandanda Day katika Mtandao wa Facebook , Daudi Mboma akizungumza wakati wa shughuli kukabidhi madawati wa shule Msingi Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam.
Afisa Elimu wa Wilaya ya Ubungo akizungumza kabla yakumkaribisha mgeni rasmi katika hafla ya kukabidhi madawati yaliyotolewa na Kandanda
Baadhi ya wajumbe kutoka Kundi la mtandao wa Facebook la Kandanda wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu; Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Anthony Peter Mavunde

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.