Habari za Punde

KOCHA LWANDAMINA 'ATUPIWA VILAGO' ZESCO, SASA KUTUA YANGA RASMI WIKI HII
FROM ∶ ZESCO UNITED FOOTBALL CLUB 7TH NOVEMBER,2016
REF; GEORGE LWANDAMINA

ZESCO United Football club would like to announce that Head Coach George Lwandamina this morning tendered in his resignation from his position with immediate effect.

The club has accepted his resignation and would like to thank him for the work and contribution during his stay.

Lwandamina joined the club in 2014 and has won two league titles, one Barclay’s cup, Charity Shield and guided the club to the 2016 edition of the CAF champion’s league semi-finals.

The club would also like to announce that Assistant coach Tenant Chembo has been appoint as acting Head Coach until the end of the season.
We would wish Lwandamina success in his new journey.

TO∶ ALL MEDIA HOUSES
Issued by 
Justin Mumba and Katebe Chengo 
Club Chief Executive Officer and Media Officer
***********************************
KOCHA wa timu ya Zesco ya Zambia, George Lwandamina, ambaye siku za hivi karibuni alizua sintofahamu ndani ya klabu yake baada ya kuripotiwa kutua Bongo na kusaini mkataba na timu ya Yanga, sasa anatarajiwa kutua nchini siku ya Jumatano kuanza mzigo baada ya kile kilichoelezwa kumalizana na klabu yake ya Zesco United.

Katika Taarifa hiyo hapo juu iliyotolea na Justin Mumba na Katebe Chengo wa Zesco, inaweka wazi kuwa wameamua rasmi kuachana na Lwandamina.

Lwandamina ambaye amekwishamalizana na uongozi wa Yanga alipotua nchini mwezi uliopita, leo anatarajiwa kuwa na kikao na waajiri wake.

“ZESCO United FC inapenda kutangaza kwamba Kocha Mkuu, George Lwandamina asubuhi hii amewasilisha barua ya kujiuzulu mara moja. Klabu imeafiki kujiuzulu kwake na inapenda kumshukuru kwa kazi na mchango wake alipokuwa kazini," walisema.

Uongozi wa Yanga unataka kumuondoa kocha Hans van der Pluijm na Wasaidizi wake wote, Juma Mwambusi, kocha wa makipa Juma Pondamali na Meneja Hafidh Saleh wote wazalendo na kuwaleta Mzambia Lwandamina atakayekuwa Kocha Mkuu, akisaidiwa na wazalendo Charles Boniface Mkwasa, Manyika Peter kocha wa makipa na Meneja, Sekilojo Chambua.

Hata hivyo, mpango huo unakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa wadau wa timu hiyo na wapenzi wanaoamini Pluijm bado ni chaguo sahihi kwa Klabu hiyo ya Wanajangwani.

Ikumbukwe wiki mbili zilizopita Pluijm alisusa kwa siku tatu kufanya kazi Yanga na kuwasilisha barua ya kujiuzulu baada ya kukerwa na taarifa za ujio wa kocha huyo mpya Mzambia. 
Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba aliingilia kati suala hilo na kufanikiwa kumrejesha kazini Pluijm. 

Waziri Mwigulu ambaye ni mpenzi na mwanachama wa Yanga, kwanza aliushauri uongozi kumrudisha Pluijm na baadaye akaenda kuzungumza na kocha huyo pia kumshauri akubali kurejea.

Baadaye akazikutanisha pande zote mbili, Pluijm na uongozi wa Yanga katika kikao ambacho inaelezwa makubaliano yalifikiwa kabla ya uongozi wa Yanga kumemuandikia barua Mholanzi huyo kumuomba radhi.

Swali ni je, Hadi ujio rasmi wa Kocha huyo, wakati Hans akiwa bado ni Kocha Mkuu wa Klabu hiyo, ni kipi kitatokea na je Uongozi tayari umeshaweka wazi kuhusu suala hilo kwa viongozi wake hao waliopo kwa sasa???

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.