Habari za Punde

LIGI KUU BARA KUENDELEA TENA VIWANJA SITA KESHO

LIGI kuu ya Tanzania bara inatarajia kuendelea kutimua vumbi hapo kesho katika viwanja sita tofauti hapa nchini ikiwa kila timu ikihitaji ushindi ili kujiweka kwenye nafasi nzuri katika msiamamo wa ligi.

Mkoani Mbeya, Mbeya City itakuwa nyumbani kuwakaribisha mabingwa watetezi wa kombe hilo timu ya soka ya Yanga katika mchezo unaotarajiwa kupigwa kwenye uwanja wa Sokoine mkoani humo.

Stand United ya mkoani Shinyanga mara baada ya kukamilisha mchezo wao wa juzi dhidi ya JKT RUVU uliochezwa kwenye uwanja Mabatini itakuwa nyumbani kuwakaribisha wekundu wa Msimbazi timu ya Simba.

Toto Africa watawakaribisha Azam Fc katika dimba la CCM kirumba na kila mmoja akiwa na kumbukumbu ya ushindi katika michezo yao iliyopita, Ruvu shooting wataikaribisha African Lyon kwenye Uwanja wa Mabatini.

Majimaji baada ya kupoteza mchezo wao dhidi ya Mbeya City mwishoni mwa wiki watavaana na JKT Ruvu katika Uwanja wa Majimaji Songea huku Tanzania Prisons watakuwa wageni kwenye Uwannja wa Nangwanda Sijaona kuvaana na Ndanda.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.