Habari za Punde

MAKADA WA CHAMA CHA MAPINDUZI CCM KATA YA LUKANGA WANAJUTA KUCHAGUA DIWANI WA KATA HIYO

 Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Abdallah Ulega akizungumza na Makada wa Chama cha Mapinduzi CCM Kata ya Lukanga Wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani.
 Diwani  kata ya Mkamba,Hassan Dunda akizungumza na Makada wa Chama cha Mapinduzi CCM Kata ya Lukanga Wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani.
 Katibu wa Tawi Kijiji cha Mkola,Shamte Ngelemange akichangia mada katika mkutano wa Makada wa Chama cha Mapinduzi CCM Kata ya Lukanga.picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.
 Baadhi ya Wazee Makada wa Chama cha Mapinduzi CCM Kata ya Lukanga Wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani,wakimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Abdallah Ulega. 
Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Abdallah Ulega akiwa katika picha ya pamoja na Makada wa Chama cha Mapinduzi CCM Kata ya Lukanga Wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani.
****************************************
MAKADA wa Chama cha Mapinduzi CCM Kata ya Lukanga wanajuta kuchagua Diwani wa Kata  hiyo  Mwarami Mketo wa Chama cha Wananchi Cuf nakudai kuwa wanajipanga upya katika uchaguzi mkuu ujao.

Hayo waliyazungunza katika Kikao cha Halmashauri kuu ya Kata ya Lukanga CCM mbele ya Mbunge wa Mkuranga Abdallah Ulega ambaye alikwenda kushuruku baada ya kuchaguliwa kuwa mbunge wa jimbo hilo.

Wakichangia mada katika mkutano huo baadhi ya wajumbe walisema kuwa walimpoteza Diwani katika kata hiyo Kwa madai kuwa miongoni mwao walifanya fitina za kuhujumu matokeo.

Akizungumza Kwa uchungu mkubwa katika mkutano huo Shamte Ngelemange alisema kuwa wanauchungu sana kukosa diwani katika kata hiyo nakudai kwamba masikitiko yake makubwa kuna wanaccm kutoka  upande wa pili walifanya hujuma za kushindwa Kwa Mgombea wao ambaye alikuwa Said Kubenea.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.