Habari za Punde

MAKAMU RAIS MGENI RASMI KATIKA MKUTANO WA WASINDIKAJI VYAKULA.

Na Eliphace Marwa-MAELEZO-Dar es salaam
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan anatarajia kuwa mgeni rasmi katika Mkutano wa Chama cha Wasindikaji Chakula Tanzania (TAFOPA).

Mkutano huo unatarajiwa kufanyika jijini Dar es Salam Desemba 3 mwaka huu unalenga kujadiliana umuhimu wa kuwa maeneo tengefu kwa viwanda vya usindikaji endelevu.

Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa TAFOPA Bibi. Suzy Laiser wakati wa mkutano na waandishi wa habari mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Aidha Bibi. Laiser aliongeza kuwa kauli mbiu ya mkutano huo ni “maeneo tengefu kwa viwanda vya usindikaji endelevu

Mkutano huo unatarajiwa kuwa na washiriki zaidi ya 100 wakiwemo Mawaziri, Wawakilishi kutoka Taasisi za Fedha, Mashirika ya Kimataifa , Vyama vya Kijamii na sekta binafsi.

Bibi. Laiser amesema kuwa washiriki wa mkutano huo watapata fursa ya kujadiliana jinsi ya kukabiliana na changamoto zinazoikabili sekta ya usindikaji wa vyakula ikiwemo ukosefu wa maeneo ili kuboresha sekta hiyo.

Bibi Laiser ameongeza kuwa hatua inalenga kuboresha shughuli za usindikaji ambapo wasindikazi katika baadhi ya maeneo wamekuwa hawazingatii kanuni na sheria zilizopo za ubora.

Amesema kuwa baada ya mkutano huo kutaundwa kikosi kazi ambacho kitakuwa na jukumu la kuhasisha rasilimali.

Mkutano huo una lenga kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wasindikaji wa bidhaa za chakula ikiwa ni pamoja na ukosefu wa viwanda vya usindikaji na kupelekea kufanya shughuli za usindikaji katika nyumba zao.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.