Habari za Punde

MAONESHO YA UTAMADUNI WA INDIA YAFUNGWA, UTAMADUNI ZA TANZANIA NA INDIA ZAWAFUNTIA WENGI

 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamisi Kigwangalla akiwasili katika maonyesho ya Utamaduni wa India yajulikanayo kama Namaste Tanzania  yaliyofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jana Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Balozi wa India nchini Tanzania Bw. Sandeep Arya.
 Balozi wa India nchini Tanzania Bw. Sandeep Arya akizungumza wakati wa kufunga maonyesho ya Utamaduni wa India (Namaste Tanzania) yaliyolenga kubadilishana utamaduni kati ya nchi ya Tanzania na India jana katika Ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam.
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamisi Kigwangalla akizungumza wakati wa kufunga maonyesho ya Utamaduni wa India (Namaste Tanzania) yaliyoonyesha ngoma kutoka Tanzania pamoja na India jana katika Ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam.
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamisi Kigwangalla (kulia) akimvalisha vazi la shingoni mmoja wa waonyesha utamaduni kutoka India kabla ya kuanza maonyesho ya Utamaduni wa India (Namaste Tanzania) jana katika Ukumbi wa Diambond Jubilee Jijini Dar es Salaam
 Kikundi cha ngoma kutoka Tanzania kikicheza ngoma wakati wa kufunga maonyesho ya Utamaduni wa India yajulikanayo kama Namaste Tanzania katika kubadilishana utamaduni kati ya Tanzania na India jana katika Ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam.
  Kikundi cha ngoma kutoka India kikifanya maonyesho ya Utamaduni wa India wakati wa kufunga maonyesho ya Utamaduni wa India (Namaste Tanzania) na kubadilishana tamaduni kati ya Tanzania na India jana katika Ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam
 Baadhi ya watu wa jamii ya India wakiangalia maonyesho ya Utamaduni wa India na Tanzania yaliyokua yakiendelea wakati wa kufunga maonyesho ya Utamaduni wa India yajulikanayo kama Namaste Tanzania Jana katika Ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamisi Kigwangalla (katikati) katika picha ya pamoja na waonyesha ngoma za Utamaduni kutoka India wakati wa maonyesho ya Utamaduni wa India (Namaste Tanzania) jana katika Ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam. Wasita kushoto ni Balozi wa India nchini Tanzania Bw. Sandeep Arya. Picha na: Genofeva Matemu - WHUSM

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.