Habari za Punde

MSHAMBULIAJI HEMEDY KUWAKOSA MTIBWA SUGAR KESHO

KOCHA mkuu wa Mbeya City fc, Kinnah Phiri, amesema mshambuliaji Hemedy Murutabose ataukosa mchezo wa kesho wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara wenyeji dhidi ya Mtibwa Sugar uliopangwa kucheza Manungu Complex Morogoro kutokana na majeraha aliyopata kwenye mchezo uliopita dhidi ya Young Africans ya Dar Es Salaam.

Akizungumza na ripota wa mtandao huu, kocha Phiri amesema kuwa maandalizi kuelekea mchezo huo yamekamilika kinachosubiriwa ni dakika 90 hapo kesho huko Manungu Complex dhidi ya wenyeji Mtibwa Sugar.

“Tuko Morogoro, tulifika hapa ijumaa usiku,siku ya jana tulifanya mazoezi kwa saa mbili na baadae vijana wakapata nafasi ya kupumzisha miili kwenye barafu,lengo likiwa ni kuwekana sawa hasa baada ya safari ndefu,leo tumefanya mazoezi ya mwisho kuhakikisha tuko fiti tayari kwa mchezo wa kesho,morali ni kubwa kambini, tutamkosa Hemedy aliyepata majeraha mchezo uliopita lakini tayari tuna watu ambao watajaza nafasi yake”, alisema.

City inakutana na Mtibwa Sugar katika mchezo huu wa kufunga duru ya kwanza ya VPL ikiwa imefanikiwa kukusanya pointi 19 na kushika nafasi ya 8 tofauti ya poingti 1 na timu hiyo ya Manungu iliyo kwenye nafasi ya 6 ikiwa imekusanya pointi 20.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.