Habari za Punde

RAIS JPM AWAONGOZA VIONGOZI NA WANANCHI KUAGA MWILI WA SPIKA MSTAAFU SAMWEL SITTA VIWANJA VYA KARIMJEE DAR

 Jeneza lenye mwili wa marehemu Samwel Sitta, likiwa kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar tayari kwa kuanza zoezi la kuagwa.
 Baadhi tu ya wananchi, Viongozi wa Kitaifa, Dini na Vyama vya Siasa wakiwa katika foleni ya kuaga mwili wa marehemu Spika Mstaafu wa Bunge la Tisa, Samwel Sitta katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.  Baada ya kumalizika shughuli hiyo katika Viwanja vya Karimjee, Mwili umesafilishwa kuelekea Bungeni mjini Dodoma,ambapo pia Waheshimiwa wabunge watapata fursa ya kutoa heshima za mwisho na baadaye kusafirishwa kuelekea mkoani Tabora kwa maziko.
 Rais Mstaafu wa awamu ya Nne, Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe, Mama Salma, wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Samwel Sitta, leo katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais Mstaafu wa awmu ya Nne, Dkt.Mohammed Gharib Bilal na mkewe, Bi Zakia Bilal, wakitoa heshima za mwisho mwili wa marehemu Samwel Sitta, leo katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
 Rais Dkt. John Pombe Magufuli, akiwafariji familia ya marehemu baada ya kutoa heshima za mwisho.
 Makamu wa Rais Mhe.Samia Suluhu Hassan, akiwafariji familia ya marehemu baada ya kutoa heshima za mwisho. KWA PICHA ZAIDI BOFYA READ MORE

 Foleni ya kuaga mwili wa marehemu Samwel Sitta.
 Foleni
 Waimbaji wa wimbo maalumu wa msiba wakiimba katika shughuli hiyo ya kuaga mwili.
 Viongozi wakiwa jukwaa kuu
 Viongozi wakiwa jukwaa kuu
 Mke wa marehemu Mama Magreth Sitta akiwa na baadhi ya wanafamilia katika shughuli hiyo.
 Rais Dkt.John Pombe Magufuli (kushoto) akiteta jambo na Rais Mstaafu wa awamu ya Nne, Jakaya Kikwete. Katikati ni Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Ali Idd
 Sehemu ya waombolezaji

 Mtoto wa marehemu akitoa shukrani
 Dkt.Magufuli na Makamu wake Samia Suluhu
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kulia) akiwa ni mwenye huzuni kubwa 
 Mama Zakia Bilal, akiteta jambo na Waziri Kairuki
 Mkuu wa Majeshi, Davis Mwamunyange (kushoto) akiteta jambo na mmoja kati ya viongozi waliofika katika shughuli hiyo.
 Sehemu ya waombolezaji waliofika katika shughuli hiyo

Waziri Kairuki akihojiwa......

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.