Habari za Punde

RAIS MAGUFULI AONGOZA WANANCHI KUAGA MWILI WA MAREHEMU MUNGAI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Waziri wa Zamani na Mbunge Mzee Joseph Mungai katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam leo Novemba 10, 2016.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimfariji mjane wa marehemu baada ya kutoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Waziri wa Zamani na Mbunge Mzee Joseph Mungai katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam leo Novemba 10, 2016

Rais Dkt. John Pombe Magufuli (wa nne kushoto), Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Mh. Benjamin Mkapa (wa tatu kushoto), Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Mohamed Gharib Bilal (wa tatu kulia), Waziri Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye (kushoto), Mke wa Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Mama Salma Kikwete (kulia) pamoja na viongozi wengine wakifatilia wasifu wa Marehemu Mzee Mungai, uliokuwa ukisomwa na Mtoto wake Mkubwa, Jimmy Mungai.

Sehemu ya familia ya aliyekuwa Waziri wa Zamani na Mbunge Mzee Joseph Mungai katika hafla ya kuuaga mwili wa marehemy katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam leo Novemba 10, 2016

Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augustine Mahiga akizungumza kwa niaba ya Serikali.Shughuli za kuaga zitaongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt John Pombe Magufuli ambaye tayari amekwishawasili ukumbini hapo na kufuatiwa na viongozi wengine waandamizi wa chama na Serikali. 

Marehemu Mungai amewahi kushika nyadhifa mbalimbali za uongozi na utumishi katika Chama na Serikali. Alikuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Mkuu wa Mkoa, Mbunge kuanzia miaka ya 1970 hadi 2010, na amekuwa Waziri katika wizara mbalimbali za Serikali ya Jamhuri ya Muungano kuanzia Awamu ya kwanza mpaka ya nne.
Viongozi Wastaafu kushoto ni Rais Mstaafu awamu ya pili Mh.William Benjamin Mkapa pamoja na Waziri Mkuu Mstaafu awamu ya Pili Mh.Frederick Sumaye na viongozi wengine waandamizi wakiwa tayari kwa kuanza kuaga mwili wa marehemu Joseph Mungai ndani ya ukumbi wa Karimjee jijini Dar. 
Viongozi Wastaafu mbalimbali wakiwa tayari kwa kuanza kuaga mwili wa marehemu Joseph Mungai ndani ya ukumbi wa Karimjee jijini Dar.
Nyimbo mbalimbali za maomboleza zikiendelea
Ndugu,jamaa na Marafiki wakiendelea kuwasilika ukumbi wa Karimjee kwa ajili ya kuaga mwili wa Marehemu Joseph Mungai, Mbunge mstaafu wa Jimbo la Mufindi aliyefariki Novemba 08, 2016 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam.
***************************************
NA IMMACULATE MAKILIKA- MAELEZO
Rais wa Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania Mheshimiwa John Magufuli leo ameongoza viongozi mbalimbali pamoja na  umma wa watanzania  katika shughuli ya kuaga mwili wa marehemu John Mungai katika viwanja vya Karim jee vilivyopo jijini Dar es salaam.
Akizungumza kwa niaba ya Serikali  wakati wa shughuli ya kuaga mwili wa marehemu, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano  wa Afrika Mashariki  Balozi Augustine Mahiga alisema kuwa  marehemu Joseph Mungai alikuwa na kipaji cha pekee cha uongozi kwa vile alipewa madaraka makubwa katika umri mdogo na katika wakati mgumu katika historia ya nchi.
“Baada tu ya Azimio la Arusha mwaka 1967 aliyekuwa  Rais wa  Awamu ya kwanza Mwl. Julius  Nyerere  alimteua marehemu Mungai  kuwa Waziri wa Kilimo wakati ambao kulikua na falsafa za  siasa ni kilimo na  kilimo ni uti wa mgongo, hakika Mwl. Nyerere alimuona ni kiongozi aliyefaa” alisema Balozi Mahiga
Ameongeza marehemu amejionesha katika ustawi wa jamii kwa kufanya shughuli mbalimbali za maendeleo ya jamii pamoja na kusaidia kaya masikini.
Kwa upande wake, mwanasiasa mkongwe nchini Kingunge Ngombale Mwiru alisema kuwa marehemu Mungai alikuwa kiongozi mahiri na mzalendo, ambaye alijenga shule  za sekondari zaidi ya saba huko mkoani Iringa ambapo baadae alizikabidhi Serikalini kwa maendeleo ya Taifa.
Naye msemaji wa Serikali ambaye ni mtoto wa marehemu Bw. Jimmy Mungai kwa niaba ya familia ameishukuru  Serikali, viongozi mbalimbali pamoja na wananchi kwa kuendelea kuwafariji katika kipindi hiki kigumu.
Marehemu Joseph Mungai amefariki Dunia ghafla Novemba 8, mwaka huu na    aliwahi kushika nyazifa mbalimbali  serikalini  ikiwemo uwaziri kwa awamu nne za serikali, pia alichaguliwa   kuwa mbunge akiwa na miaka 26 na kuwa mbunge mwenye umri mdogo kuliko wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Viongozi mbalimbali akiwemo Rais Mstaafu  wa Awamu ya Tatu mheshimiwa Benjamini Mkapa,  Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye, Makamu Mwenyeliti wa Chama cha Mapinduzi Bara Mheshimiwa Philip Mangula na  Spika wa Bunge Mstaafu  Mheshimiwa Pius Msekwa walijumuika kuaga mwili wa marehemu Joseph Mungai utakaosafirishwa kesho kuelekea mkoani Iringa na  kuzikwa jumamosi saa nane mchana. 

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.