Habari za Punde

RONALDO AWAFARIJI WAFIWA WA TIMU YA BRAZIL WA AJALI YA NDEGE

IKIWA bado dunia na ulimwengu wa soka unaomboleza msiba uliolipata Taifa la Brazil kwa ajali ya ndege iliyoua msafara wa timu ya Chapocoense wakati wakielekea kutua uwanja wa ndege wa Medellin Colombia alfajiri ya jana, Mshambuliaji wa Real Madrid, Christiano Ronaldo, ameibuka na kuwafariji wana Brazil na wachezaji waliobaki wa timu hiyo.

Ajali hiyo ya ndege iiliyokuwa imebeba abiria 81 kati ya hao 76 wamepoteza maisha huku 72 kati yao walikuwa ni sehemu ya msafara wa timu hiyo,  waliokuwa wakielekea kucheza mchezo wao wa fainali ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Amerika kusini dhidi ya Atletico Nacional ya Colombia. 

Cristiano Ronaldo ni mmoja kati ya mastaa wa soka walioguswa kwa kiasi kikubwa na msiba huo, ambapo Ronaldo ameamua kuchangia euro milioni 3 ambazo ni zaidi ya Tsh bilioni 9.6 za Kitanzania kwa timu ya Chipacoense na familia za wachezaji wa timu hiyo waliopoteza maisha. 
 
WAKATI HUO HUO: Baada ya ajali hiyo, Timu hiyo ya Chapecoense imepewa Ubingwa wa Heshima wa Michuano ya Copa Sed America, kwa kuondokewa na wachezaji wake wengi waliofariki katika ajali hiyo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.